Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Superkompyuta yatabiri England kutolewa, Messi kubeba tena Kombe la Dunia

KOMBE Pict

Muktasari:

  • Mabao mawili ya Jude Bellingham pamoja na penalti ya Harry Kane yaliisaidia timu ya Thomas Tuchel kufuzu hatua hiyo, ambapo sasa itakutana na Norway mjini Miami.

LONDON, ENGLAND: Superkompyuta iliyotengenezwa na kampuni ya ubashiri ya British Gambler imetabiri kuwa ndoto za England kutwaa Kombe la Dunia 2026 zitaishia katika hatua ya nusu fainali, huku Argentina ikitarajiwa kutetea ubingwa wake.

England ilitinga robo fainali baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mexico katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Azteca.

Mabao mawili ya Jude Bellingham pamoja na penalti ya Harry Kane yaliisaidia timu ya Thomas Tuchel kufuzu hatua hiyo, ambapo sasa itakutana na Norway mjini Miami.

Kwa mujibu wa utabiri wa superkompyuta hiyo, England itaibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Norway na kufuzu nusu fainali.

Hata hivyo, safari ya Three Lions inatarajiwa kuishia hapo baada ya kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya mabingwa watetezi Argentina.

KOMB 02

Baada ya kushindwa kutinga fainali, England inakadiriwa pia kupoteza mchezo wa kusaka mshindi wa tatu kwa mabao 2-0 dhidi ya Hispania.

Kwa mujibu wa utabiri huo, timu zitakazofuzu nusu fainali ni Ufaransa, Hispania, England na Argentina.

Ufaransa inatarajiwa kuiondoa Morocco kwa ushindi wa mabao 2-0, Hispania kuifunga Ubelgiji mabao 3-1, England kuichapa Norway bao 1-0 na Argentina kuiondoa Uswisi kwa ushindi wa mabao 2-1.

Katika hatua ya nusu fainali, Ufaransa inakadiriwa kuifunga Hispania mabao 3-2, huku Argentina ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya England.

KOMB 03

Iwapo utabiri huo utatimia, fainali ya Kombe la Dunia itakuwa marudio ya ile ya mwaka 2022 kati ya Argentina na Ufaransa, ambapo Argentina ilitwaa ubingwa kwa mikwaju ya penalti baada ya sare ya mabao 3-3.

Safari hii, superkompyuta inatabiri Argentina itaibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ufaransa katika fainali itakayochezwa Julai 19 kwenye Uwanja wa New York New Jersey.

Matokeo hayo yatamfanya nahodha Lionel Messi kuinua Kombe la Dunia kwa mara nyingine na kuiongoza Argentina kutetea taji lake.

KOMB 01

Wakati huohuo, mchambuzi wa soka wa SunSport na mshambuliaji wa zamani wa England, Troy Deeney, amesema anaamini England inaweza kuifunga Norway katika robo fainali, lakini bado anaiona Argentina ikiwa na uwezo mkubwa wa kuitoa iwapo timu hizo zitakutana katika nusu fainali.

"Natarajia tushinde dhidi ya Norway, lakini kwa kiwango cha sasa bado naiona Argentina inaweza kutufunga katika nusu fainali kama zote tutafika huko," alisema Deeney.

Aliongeza kuwa England inahitaji kuonyesha kiwango bora zaidi ikiwa inataka kutimiza ndoto ya kutwaa ubingwa wa dunia.