Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Straika Arsenal, Arteta kaanza kuchemka mapema

ARTETA Pict

Muktasari:

  • Huu unakuwa ni msimu mwingine kwa Arsenal kumaliza bila ya kupata taji lolote baada ya hivi karibuni kutolewakwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na Paris Saint-Germain na kufeli katika mashindano ya ndani.

LONDON, ENGLAND: Msimu wa 2024-25 kwa Arsenal tayari uARSENAL akili sasa ni kufanya usajili wa maana. Dirisha la usajili la majira ya kiangazi halina muda mrefu kufunguliwa na miamba hiyo ya London imeweka vipaumbekle katika kuimarisha kikosi hicho msimu ujao baada ya msimu huu kuondoka patupu kwa kukosa mataji.

Huu unakuwa ni msimu mwingine kwa Arsenal kumaliza bila ya kupata taji lolote baada ya hivi karibuni kutolewakwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na Paris Saint-Germain na kufeli katika mashindano ya ndani.

Msimu wa 2024-25 kwa Arsenal tayari umeisha, ingawa bado ina mechi mbili ambazo hazina uzito mkubwa kwani imeshajihakikishia nafasi ya pili hata ikipoteza zote.

Hata hivyo, tatizo kubwa ambalo limeisumbua kwa muda mrefu la ukosefu wa mshambuliaji wa kati asilia, huenda likaendelea kuitesa msimu ujao kutokana na mipango yao.

Tangu awasili katika kikosi cha washika mitutu hao, mwaka 2018, Kocha Mikel Arteta amesajili mshambuliaji mmoja tu ambaye ni Gabriel Jesus ambaye amekuwa nje mara kwa mara kutokana na majeraha, hali iliyomlazimu kumtumia Kai Havertz ambaye sio mshambuliaji wa kati kiasili.

Mastraika ambao wanahusishwa na washika mitutu hawa dirisha lijalo ni pamoja na Alexander Isak, Viktor Gyokeres na Benjamin Sesko, lakini wanawindwa pia na timu nyingi na Arsenal haionekani kuwekeza nguvu kuhakikisha inampata mmoja kati yao.

Hata hivyo, swali kubwa ni ikiwa Arteta ataendelea kuaminiwa, huku msimu ujao ukionekana tayari kashafeli kwa kusajili wachezaji wasiotakiwa na matarajio ya wengi ni kuboresha eneo la ushambuliaji.

Baada ya mchezo na PSG, Arteta aliulizwa kuhusu mwenendo wa timu hiyo na kama kukosekana kwa mshambuliaji asilia wa kati ndiyo sababu za kupoteza, lakini alisema anaelewa hilo lakini alishindwa kuweka wazi kama ndio sababu la anguko lao na maneno hayo hutokea tu pale pale timu inapotengeneza nafasi nyingi na kutumia chache.

Mbali ya kutokubali moja kwa moja tatizo ni safu yake ya ushambuliaji, pia anaonekana kuanza kwenda njia tofauti katika usajili wa dirisha lijalo na Arsenal inahusishwa na kiungo wa Real Sociedad, Martin Zubimendi ambaye wamekubali kumnunua kwa Pauni 51 milioni.

Arsenal Pia inaonyesha nia ya kumsajili kipa Joan Garcia kutoka Espanyol kwa karibia Pauni 30 milioni ili akampe ushindani David Raya, pia inahusishwa pia na Dean Huijsen, beki wa Bournemouth.

Usajili wa wachezaji hao unaweza ukagharimu zaidi ya Pauni 80 milioni na hadi sasa bajeti iliyopo ni Pauni 100 milioni ambayo inaweza ikaongezeka kwa kuuza wachezaji.

Jambo baya ni haionekani kama kuna wachezaji wanaoweza kuuzwa kwa kiasi kikubwa cha pesa ambazo zitatumika kufanya usajili wa straika wa kiwango cha juu, hivyo ikiwa washika mitutu hawa watamsajili Garcia, Zubimendi na Huijsen kuna uwezekano ikasajili straika wa bei rahisi au ikaachana kabisa na mpango huo.

Hata hivyo, anaamini sababu kubwa ni kuwa na kikosi kidogo kama alivyosema;

“Tulijua tangu mwanzo kikosi chetu ni kidogo sana na kuwa na kikosi kidogo sana kulimaanisha tulikuwa na wachezaji walio na uwezekano mkubwa wa kuumia, kwa sababu hiyo imewahi kutokea misimu ya nyuma,” alisema. “Na huwezi kushindania mataji ukiwa na kikosi kidogo.”

Hata hivyo, inaripotiwa pia, ni Arteta mwenyewe ndiye anapendelea kufanya kazi na kundi dogo la wachezaji, pia alikuwa na nafasi ya kusajili wachezaji wengine baada ya kuona ana kikosi chenye wachezaji wachache kabla ya msimu kuanza.

Baadhi ya mashabiki wanataka kocha huyo aondoke baada ya akushindwa kubeba mataji licha ya kuwa na kikosi bora, lakini  mabosi wa timu hiyo hawana mpango wa kumwachia wakiamini Arsenal hii ni bora kuwahi kutokea tangu mwaka 2006 walipohama  Highbury.