Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Moussa Camara atafutiwa dawa Morocco

CAMARA Pict
CAMARA Pict

Muktasari:

  • Camara ameruhusu mabao 17 katika mechi za mashindano yote ikiwamo 24 za Ligi Kuu na 12 za CAF, huku saba yakiwa ni yale ya mashuti mbali, kitu kilichofanya benchi la ufundi hasa Kocha wa Makipa, Wayne Sandilands kutumia mazoezi ya jana ya timu hiyo kumpa mbinu za kuepuka kutunguliwa tena mabao hayo dhidi ya RS Berkane.

MABAO ya mbali ambayo kipa Moussa Camara amekuwa akifungwa msimu huu yamelishtua benchi la ufundi la Simba ambalo sasa limeonekana kuwa makini kutafuta dawa ya kutibu tatizo hilo kabla ya kesho kushuka uwanjani ugenini dhidi ya RS Berkane katika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Camara ameruhusu mabao 17 katika mechi za mashindano yote ikiwamo 24 za Ligi Kuu na 12 za CAF, huku saba yakiwa ni yale ya mashuti mbali, kitu kilichofanya benchi la ufundi hasa Kocha wa Makipa, Wayne Sandilands kutumia mazoezi ya jana ya timu hiyo kumpa mbinu za kuepuka kutunguliwa tena mabao hayo dhidi ya RS Berkane.

Simba kesho itavaana na Berkane katika mechi ya mkondo wa kwanza kabla ya kurudiana nao tena wiki ijayo, huku Kombe la michuano hiyo ikiwa uwanjani na fasta benchi la timu hiyo limeonekana kujipanda mapema ili kuepuka makosa yanayoweza kuwafaidisha wapinzani wao hao wa fainali.

Jukumu la kwanza la kuhakikisha Camara harudii kosa la kufungwa mabao ya mbali linaonekana kuachiwa kwa kocha wa makipa wa Simba, Wayne Sandilands ambaye amekuwa akiwapa proramu maalum makipa wa timu hiyo kukabiliana na aina hiyo ya mashambulizi.

Sandilands amekuwa akionyesha msisitizo kwa makipa wake hasa Camara katika namna ya usimamaji langoni pindi timu inaposhambuliwa ambapo mara kwa mara amekuwa akiwahimiza kuhakikisha wanasimama katika nafasi sahihi kwa kuzingatia usawa na uelekeo wa mpigaji na pia kwa kuangalia

lango ameliacha nyuma kwa umbali gani na kutoacha nafasi kubwa ya wazi ambayo inaweza kumshawisi mpinzani mwenye mpira kupiga shuti.

Kocha huyo wa makipa wa Simba  amekuwa pia akiwapigia mipira mirefu makipa hao na wakati mwingine kuwataka wapigiane wenyewe kwa wenyewe na makipa hao ambao ni Camara, Hussein Abel na Ally Salim wamekuwa wakitimiza kwa ufasaha.

Upande wa wachezaji wa ndani pia wamekuwa waki wakifanyishwa mazoezi ya kuhakikisha hawatoi mwanya kwa wachezaji wa timu pinzani kulitazama lango kwa urahisi, jambo ambalo linaweza kuwapa ushawishi wa kupiga mashuti ya mbali.

Beki wa Simba, Shomari Kapombe amesema kuwa ni jukumu la timu nzima kushiriki katika kulinda lango na sio kipa peke yake, hivyo wanaamini  katika mechi dhidi ya RS Berkane wakiwa na tahadhari hiyo.

“Timu inaundwa na wachezaji 11 hivyo halipaswi kuwa suala la mtu mmoja au wachache kuhakikisha haifungwi bali sisi wote tuna wajibu wa kuhakikisha hilo liafanyika na kwa ufasaha.

“Kwa upande wetu tumeshafanyia kazi kasoro ambazo zimejitokeza nyuma na tutahakikisha kila kitu kinaenda sawa katika fainali,” alisema Kapombe.

Katika mabao saba ya mbali ambao Camara ametunguliwa ni mawili ni ya Coastal Union na mengine moja ya dhidi yaMashujaa, Dodoma Jiji, Fountain Gate alilitunguliwa na Ladack Chasambi na KMC, huku kwa mechi za CAF alitunguliwa robo fainali dhidi ya Al Masry ya Misry walipolala 2-0 ugenini.