Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fifa yaichomoa Congo Brazzaville kifungoni

FECOFOOT Pict

Muktasari:

  • ‎‎FIFA imetoa taarifa ya kuifungulia FECOFOOT usiku wa kuamkia leo, huku ikitoa angalizo kwa wanachama wake kurudisha ushirikiano na nchi hiyo.

Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA) limeiondolea adhabu ya kulifungia Shirikisho la soka la Congo Brazzaville (FECOFOOT).

‎‎FIFA imetoa taarifa ya kuifungulia FECOFOOT usiku wa kuamkia leo, huku ikitoa angalizo kwa wanachama wake kurudisha ushirikiano na nchi hiyo.

‎‎Taarifa ya FIFA inaeleza: Ofisi ya Baraza la FIFA kupitia uamuzi wake wa 14 Mei 2025, imeondoa adhabu ya kusimamishwa kwa FECOFOOT mara moja.

Kwa hivyo, FECOFOOT imerejeshewa haki zake zote za uanachama kwa mujibu wa sheria za FIFA.

Kwa hivyo, timu za taifa na klabu wawakilishi za FECOFOOT zinaweza kushiriki tena katika mashindano ya kimataifa.

Uamuzi huu pia unamaanisha kuwa wanachama na maafisa wa FECOFOOT wanaweza kufaidika tena na programu za maendeleo, kozi na mafunzo yanayotolewa na FIFA au CAF.

Kwa kuongeza, wanachama wa FIFA wanaweza tena kudumisha uhusiano wa michezo na FECOFOOT au timu zake.

Congo ipo kundi moja la mechi za kuwania fainali za Kombe la Dunia za 2026 na timu za Tanzania, Morocco, Zambia na Niger na adhabu ya awali ilisababisha mechi za nchi hiyo dhidi ya Tanzania na ule wa Zambia kutochezwa.