Real Madrid yaipongeza Barcelona kubeba taji

Muktasari:
- Barcelona imetwaa ubingwa baada ya kuifunga Espanyol 2-0, usiku wa kuamkia leo.
Klabu ya Real Madrid imeipongeza Barcelona kwa kutwaa ubingwa wa La Liga msimu huu 2024/25.
Barcelona imetwaa ubingwa baada ya kuifunga Espanyol 2-0, usiku wa kuamkia leo.
Real Madrid iliyokuwa bingwa msimu uliopita 2023/ 24 imetoa pongezi hizo kupitia kurasa zake zote za mitandao ya kijamii.
Ujumbe wa pongezi wa Real Madrid kwenda Barcelona unaeleza: Hongera Barcelona kwa kutwaa ubingwa 2024/25.
Barcelona imetwaa ubingwa baada ya kufikisha pointi 85 ikifuatiwa na Real Madrid yenye pointi 78, baada ya kucheza michezo 36 kila mmoja.