Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Staa Mexico atuhumiwa kwa unyanyasaji kingono

Muktasari:

  • Bravo, mwenye umri wa miaka 44, alikamatwa katika operesheni iliyofanyika katikati ya jiji la Zapopan, kufuatia malalamiko yaliyowasilishwa.

Mchezaji wa zamani wa Chivas de Guadalajara, Omar Bravo, amekamatwa Jumamosi Oktoba 4, 2025 kwa tuhuma za unyanyasaji wa kingono dhidi ya mtoto wa kike ambaye hakutajwa jina, kama ilivyothibitishwa na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Jimbo la Jalisco, magharibi mwa Mexico.

Bravo, mwenye umri wa miaka 44, alikamatwa katika operesheni iliyofanyika katikati ya jiji la Zapopan, kufuatia malalamiko yaliyowasilishwa.

“Kwa tuhuma za kuhusika katika kosa la unyanyasaji wa kingono uliozidishwa dhidi ya mtoto, maafisa wa polisi wa uchunguzi kutoka Ofisi ya Naibu Mwendesha Mashtaka anayeshughulikia masuala ya wanawake, wasichana, wavulana na familia, walifanikiwa kumtia mbaroni mwanaume anayejulikana kama Omar ‘N’,” imesomeka taarifa rasmi.

Kwa mujibu wa uchunguzi, mshambuliaji huyo wa zamani anadaiwa kumyanyasa msichana huyo mara kadhaa katika miezi ya hivi karibuni, na pia kuna tuhuma kuwa huenda alihusika na matukio mengine kama hayo hapo awali.

Omar Bravo ni mchezaji wa zamani wa soka wa Mexico aliyekuwa akicheza kama mshambuliaji. Anachukuliwa kuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi katika historia ya Chivas, akiwa na jumla ya mabao 160, na amewahi kushinda mataji mawili ya Liga MX, Interliga, na Supercopa MX.

Amezaliwa Machi 4, 1985 huko Los Mochis, Sinaloa, na ndiye mfungaji bora wa muda wote wa Chivas. Alianza kuchezea timu hiyo mwaka 2000, na katika kipindi chake cha kwanza amecheza mechi 305 na kufunga mabao 120. Umahiri wake akiwa na Chivas na Timu ya Taifa ya Mexico ulimfungulia mlango kujiunga na soka la Hispania mwaka 2008, ambapo alichezea Deportivo La Coruña.

Hata hivyo, kipindi chake Ulaya kilikuwa kifupi, na mwaka 2009 alirejea Liga MX, akichezea Tigres UANL, Cruz Azul, Atlas, na kurejea tena Chivas mara mbili. Miongoni mwa mafanikio yake ni kushiriki Kombe la Dunia 2006 nchini Ujerumani, kuwa sehemu ya kikosi cha Michezo ya Olimpiki 2004, na kushinda ubingwa wa ligi na Chivas mwaka 2006.

Akiwa na El Tri (Timu ya Taifa ya Mexico), alicheza mechi 67 na kufunga mabao 15, kabla ya kustaafu soka mwaka 2018 alipokuwa akichezea Leones Negros de la UDG.