Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Spurs yaendelea kujisogeza kwa James Trafford

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Trafford ameonekana kuwa miongoni mwa makipa ambao Spurs inawahitaji sana ili kuboresha safu yao ya ulinzi ambayo eneo la golikipa Guglielmo Vicario anatarajiwa kuondoka baada ya msimu kumalizika.

TOTTENHAM Hotspur bado inaendelea kufanya mazungumzo na Manchester City ili kumsajili kipa wa klabu hiyo na England, James Trafford, 23, katika dirisha la majira ya kiangazi.

Trafford ameonekana kuwa miongoni mwa makipa ambao Spurs inawahitaji sana ili kuboresha safu yao ya ulinzi ambayo eneo la golikipa Guglielmo Vicario anatarajiwa kuondoka baada ya msimu kumalizika.

Spurs imemhakikishia fundi huyu atakuwa kipa namba moja katika kikosi chao tofauti na ilivyo sasa akiwa na Man City na anatumika kama mbadala wa Gianluig Donnarumma ikiwa ameumia au akipumzishwa katika mashindano kama Carabao.

Mkataba wa Trafford unatarajiwa kumalizika mwaka 2030 na Man City haionekani kuwa tayari mwisho wa msimu huu kutokana na umuhimu wake hasa pale Donnarumma anapokosekana.

Hata hivyo, licha ya Man City kutoonyesha nia ya kumruhusu, Trafford mwenyewe anadaiwa kuchoshwa na hali ya kukaa benchi na anatamani sana kucheza, hivyo kuna uwezekano akawasilisha maombi ya kutaka kuondoka yeye mwenyewe.

Tangu kuanza kwa msimu huu, Trafford ambaye aliwahi kulelewa katika akademi ya Man City kabla ya kuuzwa Burnley na baadae kununuliwa tena, amecheza mechi 14 za michuano yote.


Jacobo Ramon

ARSENAL inapanga kuimarisha safu yake ya ulinzi dirisha lijalo la majira ya kiangazi na imewaweka katika orodha yao mabeki wawili raia wa Hispania, Víctor Valdepenas wa Real Madrid mwenye umri wa miaka 19, pamoja na Jacobo Ramón wa Como 1907, 21.

Valdepenas na Ramon wanatajwa wamekuwa wakitazamwa na maskauti wa Arsenal tangu mwanzo wa msimu huu na ripoti zinaonyesha kuwa wanaweza kusajiliwa na washika mitutu hao.


Elliot Anderson

NOTINGHAM Forest inataka dau kubwa linaloanzia Pauni 100 milioni ili  kumuuza kiungo wao wa kimataifa wa England, Elliot Anderson mwenye umri wa miaka 23, dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Inaelezwa klabu mbili kutoka Jiji la Manchester, Manchester United na Manchester City ndio zinapigana vikumbo kwa sasa kuiwania saini ya fundi huyu.

Anderson mwenyewe haonekani kulazimisha kuondoka na anataka timu inayomhitaji kumalizana kwanza na Forest.


Jack Grealish

EVERTON haijapanga kutumia kipengele cha kulipa Pauni 50 milioni  ili kumnunua mazima winga wa Manchester City, na England, Jack Grealish, 30, ambaye kwa sasa anacheza katika kikosi chao kwa mkopo.

Hata hivyo, Everton ina nia ya kuendelea kuipata huduma ya staa huyo na inaamini bado inaweza kufikia makubaliano mapya yatakayomuwezesha Grealish kubaki katika klabu hiyo ya Merseyside aidha kwa mkopo au kumnunua kwa bei ya chini.

Grealish ameonyesha kiwango bora sana akiwa na Everton kwa mkopo msimu kiasi cha kuishawishi timu hiyo kufikiria kumbakisha.


Gabriel Martinelli

WINGA wa kimataifa wa Brazil, Gabriel Martinelli, 24, amesisitiza kuwa bado anahitaji kuendelea kubakia Arsenal licha ya taarifa zinazodai dalili klabu hiyo inaweza kumuuza dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Martinelli anaonekana kuwa na nia ya kuendelea kuwa sehemu ya mipango ya Arsenal, akiamini bado ana nafasi muhimu katika kikosi hicho.

Hata hivyo, kwa sasa bado mazungumzo yanaendelea kati ya wawakilishi wake na vigogo wa Arsenal juu ya  mustakabali wake.


Mateo Joseph

LEEDS United iko tayari kumruhusu mshambuliaji wao wa kimataifa wa  Hispania, Mateo Joseph, 22, kuondoka dirisha la majira ya kiangazi.

Staa huyo ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo  RCD Mallorca, Hispania haonekani kuwa na nia ya kurudi England na yeye ndio aliwasilisha maombi ya kutorudi tena Leeds ili ajiunge na timu itakayompa nafasi kubwa zaidi ya kucheza.

Mkataba wa staa huyu unatarajiwa kumalizika mwaka 2028 na msimu huu amecheza mechi 30 za michuano yote.


Josh Acheampong

CHELSEA haina mpango wa kumuuza beki wao wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 19, Josh Acheampong, dirisha la usajili wa majira ya kiangazi, licha ya mchezaji huyo kupata muda mchache wa kucheza.

Chelsea bado inamuangalia  Acheampong kama sehemu ya mipango yao ya baadaye, ikiamini ana uwezo mkubwa wa kuendelea kukua na kuimarika ndani ya klabu. Taarifa nyingine zinafichua anaweza akatolewa kwa mkopo mwisho wa msimu.


Alejandro Garnacho

KOCHA mkuu wa River Plate, Eduardo Coudet ameripotiwa kufanya mawasiliano binafsi na winga wa Chelsea, Alejandro Garnacho, 21, kuhusu uwezekano wa kujiunga na klabu hiyo kwa mkopo wa mwaka mmoja.

Hata hivyo, hatua hiyo haionekani kuwa na asilimia nyingi za kufanikiwa kwani Garnacho bado anatamani kuendelea kusalia Chelsea na hata akiondoka bado kuna timu kibao barani Ulaya zinazotamani kuipata saini yake.