Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vigogo Liverpool wamepania kwa Eduardo Camavinga

Muktasari:

  • Camavinga amekuwa miongoni mwa mastaa wanaowindwa na Liverpool kwa muda mrefu na wamevutiwa zaidi na uwezo wake wa kucheza nafasi zaidi ya moja kwanjani, jambo ambalo huwa ni msaada sana pale timu inapokuwa ina idadi kubwa ya majeruhi wanaocheza nafasi mbalimbali.

LIVERPOOL inajiandaa kikamilifu kwa ajili ya kuwasilisha ofa kwenda Real Madrid baada ya klabu hiyo kueleza kwamba ipo tayari kusikiliza ofa kwa ajili ya kumuuza kiungo wa Ufaransa, Eduardo Camavinga, 23.

Camavinga amekuwa miongoni mwa mastaa wanaowindwa na Liverpool kwa muda mrefu na wamevutiwa zaidi na uwezo wake wa kucheza nafasi zaidi ya moja kwanjani, jambo ambalo huwa ni msaada sana pale timu inapokuwa ina idadi kubwa ya majeruhi wanaocheza nafasi mbalimbali.

Inaelezwa Madrid inahitaji zaidi ya Euro 90 milioni ili kumwachia fundi huyu kiasi ambacho timu nyingi zinaonekana kusita kukilipa. Liverpool inapambana kusuka kikosi chao upya baada ya kufanya vibaya msimu huu na moja kati ya changamoto ikionekana kuwa ni safu yao ya kiungo.

Mkataba wa sasa wa Camavinga unatarajiwa kumalizika 2029 na tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 25 za michuano yote na kutoa asisti moja.


Bernardo Silva

BARCELONA na Juventus ni miongoni mwa timu zinazotaka kumsajili kiungo wa Manchester City, Bernardo Silva, 31, kwa uhamisho wa bure dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Silva amekuwa mmoja wa wachezaji muhimu katika mafanikio ya Manchester City, akisifika kwa ubunifu na uwezo wa kumiliki mpira pamoja na kufanya maamuzi sahihi. Mkataba wake wa sasa unamaliziika mwisho wa msimu huu na taarifa zinaeleza wazi fundi huyo ataondoka.


Manuel Ugarte

JUVENTUS inaamini kufuzu kwao Ligi ya Mabingwa Ulaya ndio kutawaweka katika nafasi nzuri ya kumsajili kiungo wa Manchester United, Manuel Ugarte, 24, dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Ugarte, anayekipiga Man United, ni miongoni mwa wachezaji wanaotarajiwa kuuzwa ifikapo dirisha lijalo na ada yake ya uhamisho inaweza kuwa ni Pauni 35 milioni. Juventus inaamini uwepo wao Ligi ya Mabingwa unaweza kuwa kivutio kikubwa kwa mchezaji huyo.


Yan Diomande

ARSENAL imeipiku Liverpool katika mbio za kumsajili winga wa RB Leipzig, Yan Diomande, 19, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Diomande anaendelea kuvutia klabu kubwa Ulaya kutokana na kiwango bora alichoonyesha msimu huu. Arsenal inadaiwa ilishamaliza kufanya mazungumzo binafsi na mchezaji huyo na sasa ipo katika mazungumzo na Leipzig juu ya ada ya uhamisho.


Cristian Romero

TOTTENHAM Hotspur imesisitiza haitakubali ofa yoyote chini ya Euro 50 milioni kutoka kwa timu zitakazohitaji huduma ya nahodha wao, Cristian Romero. Beki huyo wa kimataifa wa Argentina anawaniwa na Atletico Madrid, ambayo inataka kuimarisha safu yake ya ulinzi kuelekea msimu ujao. Kwa sasa Romero ni mhimili muhimu katika safu ya ulinzi wa Tottenham jambo linaloifanya Spurs kutaka kumuuza kwa pesa nyingi.


Vinicius Junior

IKIWA mshambuliaji Vinicius Junior, 25, ataamua kuondoka Real Madrid dirisha lijalo la majira ya kiangazi, sehemu pekee anayodaiwa anatamani kwenda ni aidha Paris Saint-Germain au moja ya timu kubwa England na siyo Saudi Arabia kama ilivyoripotiwa mara kadhaa. Vinicius ni mmoja wa wachezaji muhimu zaidi Real Madrid kwa sasa, lakini mara kadhaa amedaiwa kuwa huenda akaondoka mwisho wa msimu huu kwa sababu hana furaha.


Karim Coulibaly

NEWCASTLE ipo tayari kuingia kwenye ushindani mkali na klabu nyingine Ulaya katika mbio za kumsajili beki chipukizi wa Werder Bremen, Karim Coulibaly, 18. Coulibaly, ameonekana kuwa mmoja wa mabeki bora Bundesliga licha ya umri wake mdogo jambo lililozivutia timu nyingi. Mbali ya Newcastle, Bayern Munich nayo inahitaji huduma ya fundi huyu na ipo tayari kulipa Euro 30 milioni.


Maghnes Akliouche

LIVERPOOL na Manchester United zimeongeza juhudi katika mbio za kumsajili winga wa kimataifa wa Ufaransa, Maghnes Akliouche, 24, anayekipiga AS Monaco. Akliouche amekuwa katika rada za vigogo Ulaya tangu mwaka jana lakini changamoto kubwa ni Monaco haikutaka kumwachia katikati ya msimu. Man United na Liverpool huenda zikahitajika kutoa zaidi ya Euro 60 milioni ili kufanikisha mchakato huo.