Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Slot awavaa wachambuzi

SLOT Pict

Muktasari:

  • Liverpool ilitumia fedha nyingi dirisha la usajili la majira ya kiangazi, ikimsajili Alexander Isak na Florian Wirtz.

LIVERPOOL, ENGLAND: KOCHA wa Liverpool, Arne Slot amelalamikia wachambuzi wanaozungumzia sana wachezaji wake wapya na gharama zilizotumika kuwasajili jambo ambalo haoni kama lina afya kwa ukuaji wao.

Liverpool ilitumia fedha nyingi dirisha la usajili la majira ya kiangazi, ikimsajili Alexander Isak na Florian Wirtz.

Isak aliweka rekodi ya uhamisho ya England ya Pauni 125 milioni wakati Wirtz aliweka ya Pauni 116 miloni.

Wirtz ameanza kila mchezo wa ligi msimu huu ingawa amekuwa akihangaika kuzoea maisha ya Ligi Kuu England, wakati Isak akianza katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya juzi dhidi ya Atletico.

Slot alilalamikia umakini unaoelekezwa kwa wachezaji wapya, akieleza wachambuzi wanaounga mkono klabu nyingine wamekuwa wakitaja matumizi ya Pauni 450 milioni yaliyofanywa hvi karibuni bila kukumbuka Liverpool pia imeuza wachezaji kwa Pauni 300 milioni.

Kocha huyo Mholanzi pia alieleza mbali na wachezaji waliosajiliwa kwa pesa kubwa watu lazima waelewe hata wachezaji waliopo katika kikosi sasa nao thamani zao ni kubwa.

Slot alimtaja kiungo wake Dominik Szoboszlai, ambaye amekuwa mchezaji bora wa kikosi hicho tangu kuanza kwa msimu huu, angeuzwa kesho basi bei yake isingekuwa chini ya Pauni 100 milioni.

"Wachezaji tuliowaleta kweli wamegharimu fedha nyingi, lakini sasa wanacheza sambamba na wachezaji wengine wenye thamani sawa. Ndiyo, tukitaka kuimarisha kikosi, mara nyingi tunalazimika kutumia kiasi hicho cha fedha, lakini hiyo haimaanishi wachezaji waliosajiliwa ndio ghali zaidi kikosini kwa sababu kuna wengine kama Dominik Szoboszlai tukimuuza kesho, thamani yake ni Pauni 100 milioni."

Szoboszlai ameanza kila mchezo wa ligi msimu huu na licha ya kucheza kama kiungo nafasi yake mama, alicheza kama beki wa kulia dhidi ya Newcastle United, Arsenal na Burnley.

Ameonyesha kiwango kizuri katika nafasi hiyo na hata kufunga bao la ushindi dhidi ya Arsenal mwezi uliopita.