Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maswali magumu inayoenda kuulizwa England na Mexico

Muktasari:

  • Hiyo ni mechi kati ya England dhidi ya wenyeji wenza, Mexico, ambayo inapigwa katika dimba la Azteca lililopo kwenye mwinuko unaowatesa wachezaji wa timu ngeni kila mara.

MEXICO CITY, MEXICO: HATIMAYE imefika. Unapofikiria kupanda kitandani leo usiku kumbuka kwamba ifikapo saa 9:00 usiku ile mechi ya kibishi inapigwa.

Hiyo ni mechi kati ya England dhidi ya wenyeji wenza, Mexico, ambayo inapigwa katika dimba la Azteca lililopo kwenye mwinuko unaowatesa wachezaji wa timu ngeni kila mara.

Ni katika uwanja huo ambao England ilichapwa na Argentina mabao 2-1 katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Dunia 1986, Diego Maradona akitupia moja ya mabao yanayotajwa kuwa bora la muda wote katika mashindano hayo.

Achana na ukweli kwamba alitangulia kuwafunga lile lililokuja kupata umaarufu kama bao la ‘Mkono wa Mungu’, lakini lile la apili ndilo lililokuwa tamu zaidi kwani aliwafunga tela mastaa kibao wa England, kisha akamchambua na kipa wao Peter Shilton na kufunga kirahisi bao la pili.

Na leo, England wanarudi katika uwanja huohuo ambao umekuwa ukizitisha timu nyingi katika mashindano mbalimbali ya kimataifa, lakini kwa wenyeji ni dimba la kawaida kabisa kwao kwani rekodi zao si haba.

Kuna vijisehemu saba muhimu vinavyoweza kuamua mchezo huo wa hatua ya 16 Bora ya Kombe la Dunia 2026, lakini swali kubwa likiwa ni je, Mexico wataendelea kung’ara mbele ya mashabiki wao wa nyumbani au England wataweza kuinua kiwango na kusonga hadi robo fainali? Hivi hapa vijisehemu sita muhimu vinavyoweza kuamua mchezo huu, na tuwemo!

Mchezo huo ukichezwa katika Uwanja wa Azteca uliopo kwenye mwinuko wa juu na mbele ya umati mkubwa wa mashabiki wa nyumbani, Mexico watataka kuendeleza kampeni ya kuvutia ya Kombe la Dunia 2026 ambayo bado haijawahi kuona wakiruhusu bao.

Timu hiyo hawajawahi kupoteza mchezo wa Kombe la Dunia ndani Azteca katika mechi 10 zilizopita ilizocheza hapo, huku pia ikiwa imepoteza mechi mbili pekee kati ya 89 za mashindano ilizocheza uwanjani hapo. England haina kumbukumbu nzuri kuhusu Azteca. Huo utakuwa mchezo  wa kwanza baada ya miaka 40, kwani mara ya mwisho walipocheza ilikuwa katika Kombe la Dunia 1986, ambapo walifungwa na Argentina katika mchezo uliokuwa wa ‘mbabe’ Maradona.


KUNA UWANJA MGUMU KULIKO AZTECA ENGLAND?

Ilipopangwa njia ya England kuelekea fainali ya Kombe la Dunia, ilifahamika kila wakati kwamba kuna uwezekano mkubwa ingekutana na Mexico Azteca. Siyo tu kwamba uwanja huo umeshuhudia mechi nyingi zaidi za Kombe la Dunia kwa wanaume kuliko uwanja mwingine wowote katika historia ya mashindano hayo (23), pia ni uwanja ambao Mexico wamefurahia rekodi ya ajabu.

Wameshinda mechi zote tatu walizocheza uwanjani hapo Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Afrika Kusini, Czechia na Ecuador, na hivyo kuendeleza rekodi ya kutofungwa Azteca katika historia ya Kombe la Dunia hadi mechi 10 (ushindi mara nane na sare mbili). Lakini rekodi yao bora Azteca siyo ya Kombe la Dunia pekee, bali Mexico wamecheza mechi 89 za mashindano uwanjani hapo katika historia na wamepoteza mara mbili tu.

Vipigo hivyo viwili vilitokea katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia mwezi Juni 2001 (dhidi ya Costa Rica) na Septemba 2013 (dhidi ya Honduras). Zote ziliisha kwa mabao 2-1, na katika zote Mexico walitangulia kufunga ndani ya dakika saba, wakiongoza hadi mapumziko lakini wakashindwa kushikilia uongozi wao.


VIPIGO VYA MEXICO AZTECA

Vipigo hivyo vinaonekana kuwa vya muda mrefu sana. Tangu wakati huo Mexico wamecheza mechi 22 za mashindano Azteca na hawajapoteza hata moja, wakishinda 16 na kutoka sare sita. Lakini, ubora wa wapinzani wao pia unapaswa kuzingatiwa.

Ukitazama nafasi ya Fifa ya wapinzani wao wakati wa kila moja ya mechi hizo 22, wastani wa nafasi ya wapinzani ilikuwa ya 57 duniani.

Ni mechi mbili tu kati ya hizo zilizochezwa dhidi ya timu zilizo ndani ya 20 bora ya Fifa wakati huo – Marekani walikuwa wa 13 Machi 2022 (0-0) na Costa Rica walikuwa wa 19 Machi 2017 (2-0), huku ni mechi nne pekee zilikuwa ndani ya 30 bora. Mechi 15 kati ya 22 zilikuwa dhidi ya wapinzani waliokuwa nafasi ya 50 au chini wakati huo.

England watacheza mchezo wao wa tatu Azteca baada ya kucheza mara mbili uwanjani hapo katika Kombe la Dunia 1986, wakiwa na matokeo mchanganyiko. Simba Watatu waliifunga Paraguay 3-0 katika raundi ya pili kabla ya kupata moja ya vipigo vyao maarufu zaidi katika historia ya Kombe la Dunia kutokana na bao la ‘Mkono wa Mungu’ la Maradona, likifuatiwa na bao lake la pili dakika nne baadaye ambalo mara nyingi huitwa “Bao la Karne”.

Kitu kingine ambacho England watakabiliana nacho Azteca ni mwinuko. Uwanja uko takriban mita 2,200 juu ya usawa wa bahari. Linganisha hilo na Uwanja wa West Bromwich Albion, The Hawthorns kule England ambao uko mita 168 juu ya usawa wa bahari, ukiwa ndio uwanja ulio juu zaidi katika soka la kulipwa England.

Bila shaka, rekodi nzuri ya Mexico uwanjani hapo siyo kwa sababu ya mwinuko pekee. Walimshinda Ecuador katika raundi iliyopita uwanjani hapo, timu ya taifa ambayo kwa kawaida hucheza mechi za nyumbani kwenye mwinuko wa takriban mita 2,743 huko kwao Quito, Ecuador.


JE, MWINUKO UTAATHIRI KWELI?

Kwa kifupi, ndiyo. Kocha na mwandishi maarufu wa michezo, Steve Magness, hivi karibuni alizungumzia changamoto ambazo England wanaweza kukutana nazo Azteca akisema: “Katika futi 7,000, VO2max (uwezo wa mwili kutumia oksijeni wakati wa kukimbia) itashuka takriban asilimia 10–13. Tuliona hili katika mashindano ya riadha ya Olimpiki ya 1968. Na utendaji hushuka takriban kati ya asilimia tano na sita kulingana na umbali wa mbio.”

Anaongeza kuwa, “umbali wa jumla na kukimbia kwa kasi kubwa hushuka sana. Asilimia kati ya tatu na tisa kwa wa mara ya kwanza, 10 hadi 15 kwa mara ya pili. Kadri mwinuko unavyoongezeka, athari inakuwa kubwa. Kadri mtu hajazoea, ndivyo athari inavyokuwa kubwa.”

Takwimu za Opta kutoka Kombe hili la Dunia zinaonekana kuunga mkono hilo. Ukitazama mechi za makundi zilizochezwa katika mashindano hayo kwenye viwanja vyote, Azteca ilirekodi wastani wa chini kabisa wa umbali uliokimbiwa kwa kila mchezo na timu zote mbili kwa pamoja (kilomita 208.5), idadi ndogo zaidi ya mbio za kasi kubwa kwa kila mchezo (500.3) na wastani wa chini zaidi wa sprinti kwa kila mchezo (113.0). Athari inaweza isiwe dhahiri sana ikiwa England wataweza kumiliki mpira na kuepuka kukimbizana na Mexico. Hadi sasa katika mashindano hayo, kikosi hicho cha Thomas Tuchel kimekuwa na wastani wa umiliki wa mpira wa asilimia 63.8 ikiwa ni juu sana kuliko wastani wa Mexico wa 48.4, lakini hali ya mchezo huenda imechangia (Mexico bado hawajawahi kuwa nyuma kwenye alama).


ENGLAND WATASTAHIMILI MWANZO MWISHO?

Itakumbukwa kwamba ule muda wa kupoza koo (hydration break) wa kwanza ulikuwa katika dakika ya 25 ya mchezo wa raundi ya 32 kati ya Mexico na Ecuador, ambapo Waequador walihitaji “kuongeza maji mwilini” zaidi kuliko wenyeji. Mexico walikuwa tayari wanaongoza bao 1-0 kupitia Julian Quinones dakika tatu tu kabla, lakini walikuwa wamedhibiti mchezo kikamilifu.

Pia walikuwa tayari wamepiga mashuti saba, huku Ecuador wakiwa na jaribio moja tu langoni, na Mexico walikuwa na idadi karibu mara mbili ya mipira iliyoguswa katika eneo la mwisho ikiwa ni 37 dhidi ya 19 ya wapinzani wao. Mexico walifunga bao la pili muda mfupi baada ya hydration break kupitia Raul Jimenez, na hakukuwa na njia ya kurudi kwa Ecuador waliokuwa wameshindwa kabisa kupambana. England walikumbana na hali tofauti dhidi ya DR Congo majuzi kule Marekani, ambapo walizidiwa kabisa mwanzoni kabla ya hydration break kuwasaidia kujipanga upya. Walitawala mpira lakini hawakupiga shuti hata moja mwanzoni, na waliruhusu bao kupitia shuti pekee lililolenga lango la DR Congo.

Baada ya mapumziko ya kipindi cha kwanza, England walipiga mashuti manane ndani ya dakika 26 (pamoja na muda wa nyongeza), lakini walizuiwa na uhodari wa kipa Lionel Mpasi. England hawawezi kumudu kuanza vibaya katika mchezo huo huko Azteca. Tofauti na Ecuador, ambao wamezoea mwinuko, kikosi cha Tuchel hakitataka kuwa nyuma na kukimbizana na mchezo.


WATAWEZA KUVUNJA ULINZI WA MEXICO?

Mexico hawajawa na matatizo makubwa dhidi ya wapinzani wao hadi sasa katika Kombe la Dunia 2026. Hata hivyo, kundi lao lilionekana kuwa la kiwango cha chini kwa mujibu wa Opta, lakini bado wamefanya vizuri kiulinzi. Bado hawajaruhusu bao katika Kombe hili la Dunia, wakitoka na clean sheet dhidi ya Afrika Kusini, Korea Kusini na Czechia kwenye makundi kabla ya nyingine dhidi ya Ecuador katika raundi ya 32.

Mexico ni timu ya pili tangu 1994 kuwa na clean sheet katika mechi nne za kwanza za Kombe la Dunia baada ya Uswisi 2006 na wanaweza kuwa timu ya pili katika historia ya Kombe la Dunia kuwa nazo katika mechi tano za kwanza za shindano moja, baada ya Italia 990 (5), ambao walimaliza nafasi ya tatu. Kikosi cha Mexico chini ya Javier Aguirre kimeruhusu mashuti matano tu yaliyolenga lango katika mechi nne, huku wapinzani wao wakipata wastani wa kuruhusu bao wa 0.56 kwa mchezo. Mexico wamekuwa wakitumia asilimia 65 ya muda wakiwa mbele kwenye alama katika mashindano haya na bado hawajawahi kuwa nyuma. Hata hivyo, hawakuonekana kujilinda sana hadi walipoongoza 2-0 dhidi ya Ecuador. Kama Mexico wataanza kwa kufunga dhidi ya England, huenda ikawa changamoto nyingine kwa Simba Watatu.


KUTUMIA KIKOSI CHA NYOTA 26

Kwa kuzingatia uchovu wa mwinuko, huenda hii ikawa mechi ambayo England watatumia kina cha kikosi chao, ikizingatiwa kwamba ulinzi wao haujawa thabiti katika mashindano hayo. Kila mchezo kati ya minne wameanza na safu tofauti ya ulinzi ya wachezaji wanne.

Nafasi ya beki wa kulia ndiyo yenye changamoto zaidi kwa Tuchel, ambapo Tino Livramento aliondoka kwenye kikosi kabla ya mashindano kuanza, majeraha ya Reece James nayo yamerudi tena na kumtoa nje, huku Jarell Quansah pia akiumia baada ya kuingia kuchukua nafasi yake dhidi ya Panama.

Djed Spence alipewa nafasi ya beki wa kulia dhidi ya DR Congo lakini hakuwa na athari kubwa kabla ya Declan Rice kuhamishiwa huko kwa dakika 20 za mwisho. Utakuwa uamuzi wa ajabu kumtoa Rice katika eneo la kiungo wa kati, lakini inawezekana, jambo ambalo linaweza kumaanisha Kobbie Mainoo akaanza kwa mara ya kwanza katika mashindano hayo.

Harry Kane amecheza karibu dakika zote katika kampeni ya England, huku Ollie Watkins akiwa amecheza dakika sita pekee kama mbadala. Ivan Toney hajacheza kabisa, lakini huenda hii ndiyo mechi ya kumuona akicheza pamoja na Kane ikiwa mambo yatakwenda vibaya. Mexico tayari wamewapa nafasi wachezaji 25 kati ya 26 wa kikosi chao katika mashindano hayo.


JE, HARRY ATAWAOKOA TENA?

Kama mambo yote yatashindikana, basi tumaini ni Harry Kane kufunga bao, sivyo? Kane alikuwa tena shujaa wa England Jumatano iliyopita  waliporudi kutoka nyuma na kushinda mabao 2-1 dhidi ya DR Congo.

Nahodha huyo alifunga mabao yake ya 12 na 13 katika historia ya Kombe la Dunia na kuendelea kuwa mfungaji bora wa taifa lake katika mashindano hayo na sasa ana mabao 84 kwa England kwa jumla, 31 zaidi ya Wayne Rooney (53). Nyota huyo wa Bayen Munich ameendelea kuwa chanzo cha uhakika cha mabao katika mashindano makubwa. Tangu Kombe la Dunia 2018, mabao 20 kati ya 52 ya England katika mashindano makubwa yamefungwa na Kane (takriban asilimia 38.5), huku Jude Bellingham akiwa wa pili kwa mabao matano. Hakuna mchezaji mwingine katika Kombe hili la Dunia aliye katika kiwango bora cha ufungaji kama Kane, ambapo straika huyo anaweza kufikisha miaka 33 mwezi huu, lakini haonyeshi dalili ya kupungua uwezo wake.

Bao lake la pili dhidi ya DR Congo lilimfikisha kwenye mabao 72 katika mechi 62 kwa klabu na taifa tangu Agosti Mosi, 2025, zaidi kuliko mchezaji mwingine yeyote kwenye kikosi cha Kombe hili la Dunia. Zaidi ya hapo, mabao hayo yametokana na mashuti yenye thamani ya uwezekano wa bao kufungwa kutoka kwenye nafasi (xG) ya 50.2 akizidi matarajio kwa mabao 22. Mexico watakuwa timu ya 52 tofauti ambayo Kane amecheza nayo akiitumia England, na amefunga dhidi ya 36 kati ya 51 zilizopita. Wachache wanaweza kupinga uwezekano wa kuongeza timu nyingine mwathirika kutoka kwake mwishoni mwa wiki hii.