Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Slot anatafuta mtu Liverpool

SLOT Pict

Muktasari:

  • Slot ambaye ni raia wa Uholanzi, amempoteza mmoja wa wasaidizi wake muhimu mwisho wa msimu huu na sasa anataka msaidizi mpya na tayari ana majina matatu likiwamo na lejendi wa timu hiyo, Dirk Kuyt.

LIVERPOO, ENGLAND: KOCHA wa Liverpool, Arne Slot, anatafuta msaidizi mpya baada ya John Heitinga kuachana na timu hiyo na kutua Ajax ambako amepata ajira ya kuwa kocha mkuu.

Slot ambaye ni raia wa Uholanzi, amempoteza mmoja wa wasaidizi wake muhimu mwisho wa msimu huu na sasa anataka msaidizi mpya na tayari ana majina matatu likiwamo na lejendi wa timu hiyo, Dirk Kuyt.

Kuyt, ambaye aliwahi kuchezea Liverpool kwa miaka sita, amejumuishwa kwenye orodha fupi ya makocha wanaoweza kupewa nafasi hiyo licha ya kutofanya vizuri katika ajira yake ya sasa.

Mshambuliaji huyo wa zamani, aliyewahi kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa akiitumikia Liverpool, kwa sasa anaifundisha Beerschot iliyokuwa ikishiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji na sasa imeshashuka baada ya kufanya vibaya msimu uliomalizika.

Mbali ya Kuyt, makocha wengine ambao Slot amewaweka katika orodha ni Marino Pusic aliyekuwa msaidizi wake huko AZ Alkmaar na Feyenoord ambaye hivi karibuni amejiuzulu nafasi yake kama kocha wa Shakhtar Donetsk. Licha ya kujiuzulu Pusic alishinda mataji mawili ya ndani akiwa na timu hiyo.

Gazeti la Liverpool Echo pia limeripoti kuwa Etienne Reijnen naye ni miongoni mwa makocha wanaoweza kupewa ajira hiyo.

Reijnen ni kocha msaidizi wa sasa wa Feyenoord na alitarajiwa kumfuata Slot msimu uliopita, lakini mipango ilikwama kutokana na matatizo ya kibali cha kazi.

Licha ya mabadiliko haya katika benchi la ufundi, Slot alimpongeza  Heitinga kwa nafasi hiyo aliyoipata.

Ajax walikuwa wakitafuta kocha mpya baada ya Francesco Farioli kujiuzulu mwishoni mwa msimu. Timu hiyo ilipoteza ubingwa wa Eredivisie kwa PSV baada ya kupitwa katika dakika za mwishoni licha ya kuongoza kwa pointi tisa hadi mechi tano za mwisho za msimu.