Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Slot aipa onyo Real Madrid

Muktasari:

  • Real Madrid iliwasiliana na Liverpool usiku wa kuamkia Mwaka Mpya kuhusiana na kumsajili Trent  Januari hii, lakini Liverpool walikataa mara moja. Hata hivyo, kwa kuwa mkataba wa beki huyo unamalizika msimu huu, huenda Madrid ikampata bure wakati huo.

LIVERPOOL, ENGLAND: BAADA ya Liverpool kuripotiwa kumpa ofa ya mkataba wa miaka mitano utakaomwezesha kukunja Pauni 78 milioni, mchezaji wao Trent Alexander-Arnold, kocha wa timu hiyo Arne Slot amewaonya Real Madrid kwamba juhudi zao za kumnasa beki huyo hazitokuwa rahisi akitolea mfano wa kushindwa kwao kumshawishi Steven Gerrard kujiunga nao hapo zamani.

Real Madrid iliwasiliana na Liverpool usiku wa kuamkia Mwaka Mpya kuhusiana na kumsajili Trent  Januari hii, lakini Liverpool walikataa mara moja. Hata hivyo, kwa kuwa mkataba wa beki huyo unamalizika msimu huu, huenda Madrid ikampata bure wakati huo.

Alipoulizwa na waandishi wa habari iwapo anahofia kwamba Madrid inaweza kumchukua Trent kwa sababu ya ushawishi wao, Slot alisema: “Kulikuwa na mchezaji mmoja (Gerrard) ambaye walitamani sana kuwa naye, lakini hawakumpata. Unamjua vizuri kuliko mimi. Kwa hivyo, hilo limeshatokea.”

Jose Mourinho alijaribu kumsajili Gerrard kwenda Real Madrid mwaka 2010, lakini lejendi huyo wa Liverpool alikataa.

 Mapema mwaka huu, Gerrard alizungumzia dili hilo akisema: “Nilipokea ofa kutoka Real Madrid na Chelsea, lakini moyo wangu ulikuwa daima kwa Liverpool. Sikuwahi kujuta kwa uamuzi wangu. Ikiwa muda utarudi nyuma, nitafanya vivyo hivyo.”

Kama ilivyokuwa kwa Gerrard, Alexander-Arnold ni mhitimu wa akademi ya Liverpool hivyo huenda naye akafuata nyayo zake.

Trent akiondoka atafuata nyayo za mastaa wa timu hiyo wa zamani kama Steve McManaman na Michael Owen.