Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Guardiola kubeba wawili kwa Pauni 180 milioni

GUARDIOLA Pict

Muktasari:

  • Man City ipo kwenye mpango wa kukijenga kikosi cha kocha Pep Guardiola na kuwekeza Pauni 180 milioni huku lengo likiwa ni kuwanasa viungo wachezaji, Wirtz wa Bayer Leverkusen na Reijnders wa AC Milan.

MANCHESTER, ENGLAND: NDO hivyo. Manchester City ipo tayari kutumia Pauni 180 milioni ili kuwanasa Florian Wirtz na Tijjani Reijnders kabla ya kuanza kwa fainali za Kombe la Dunia la Klabu mwezi ujao.

Man City ipo kwenye mpango wa kukijenga kikosi cha kocha Pep Guardiola na kuwekeza Pauni 180 milioni huku lengo likiwa ni kuwanasa viungo wachezaji, Wirtz wa Bayer Leverkusen na Reijnders wa AC Milan.

Leverkusen inahitaji zaidi ya Pauni 100 milioni ili kumwachia staa huyo wa Ujerumani na hilo halihusiani na mpango wa Man City wa kutaka kumwongeza James McAtee mwenye thamani ya Pauni 25 milioni kuwa sehemu ya dili hilo. Na Milan iliweka wazi kwamba itazigharimu pesa nyingi klabu zinazomtaka kiungo wake wa ubunifu, Reijnders, ikifichua kwamba itahitaji Pauni 56.3 milioni.

Wachezaji wote hao wanaweza kuhusika kwenye mechi za kufuzu Kombe la Dunia mwezi ujao na kocha Guardiola atahitaji dili za wachezaji wengi zifanyike kama ya kikosi chake cha Man City kwenda kushiriki Kombe la Dunia la Klabu litakalofanyika Marekani.

Man City inaamini inaweza kumudu mishahara ya wachezaji hao wawili kwa sababu itakuwa na ziada inayozidi Pauni 350,0000 kwa wiki, ambayo ilikuwa ikimlipa Kevin De Bruyne, ambaye ataondoka mwisho wa msimu huu baada ya mkataba wake kufika tamati huko Etihad.

Wirtz, 22, analipwa mshahara pungufu ya Pauni 80,000 kwa wiki huko kwenye kikosi cha Leverkusen na mchezaji huyo anatazamwa kama mrithi sahihi wa De Bruyne. Na Reijnders, 26, ambaye alisaini mkataba mpya wa miaka mitano kwenye kikosi cha Milan, Machi mwaka huu, mshahara wake ni Pauni 96,000 kwa wiki.