Skauti Liverpool afunguka dili la Guehi
Muktasari:
- Mbali yakuwa mbadala wa Van Dijk, skauti huyo pia amesema kwa sasa usajili wa Guehi pia ni kwa ajili ya kuziba pengo la Ibrahima Konate ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu.
LIVERPOOL, ENGLAND: SKAUTI wa Liverpool, Stewart Downin ambaye kazi yake ni kutambua na kupendekeza wachezaji ameweka wazi kwamba beki wa Crystal Palace Marc Guehi ambaye anahitajika na Liverpool anasajiliwa kwa ajili ya kuziba pengo la Virgil van Dijk.
Mbali yakuwa mbadala wa Van Dijk, skauti huyo pia amesema kwa sasa usajili wa Guehi pia ni kwa ajili ya kuziba pengo la Ibrahima Konate ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa Jumamosi usiku, Liverpool iliwasilisha ofa ya Pauni 35 milioni kwa Crystal Palace ili kumsajili Guehi.
Palace italazimika kumuuza Guehi kwa sababu mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu na hadi bado hajakubali kusaini mkataba mpya kama ilivyo kwa Konate.
"Nadhani Guehi anakuja kama mchezaji wa kuongeza nguvu, na kwa mtazamo wangu baada ya miaka michache ataibeba nafasi ya Van Dijk, naamini hilo. Nilidhani wangeshamchukua katika dirisha la majira ya joto yaliyopita kwa kuwa walihusishwa naye mara nyingi. Hali ya Konaté ni ngumu kwa sababu kama ataendelea kukataa kusaini mkataba mpya, tutalazimika kumuuza ili kuepuka kumwachia bure. Anaweza kuondoka sasa au Januari. Pengine tukashuhudia mshangao mwishoni mwa dirisha hili la usajili,"alisema Downing na kuongeza,
"Pia kwa asilimia kubwa Konate anaweza akaondoka, na Guehi ni mbadala mzuri kwa kweli. Si mchezaji mbaya, na kwa ofa hiyo iliyowasilishwa ikiwa itakubaliwa nadhani ni dili zuri, ninaamini litakamilika kama sio sasa basi hata Januari."
Hata hivyo, dili la beki huyo litatakiwa kabla ya saa sita usiku wa leo ambapo dirisha la usajili litakuwa linafungwa.
Baadhi ya taarifa zinadai, Palace pia inaweza kumchukua Joe Gomez na pesa kidogo kama sehemu ya makubaliano ya kumruhusu Guehi kwenda Liverpool.