Siri ya Tattoo ya Messi mguuni

MIAMI, MAREKANI. STAA wa Inter Miami, Lionel Messi amesisitiza tattoo yake aliyochora mguuni ni maalumu kwa ajili ya timu yake ya zamani Barcelona.
Messi, 36, alikipiga Barcelona kwa muda wa miaka 21 kabla ya kutimkia Paris Saint-Germain mwaka 2021 kutokana na mataizo ya kiuchumi.
Lakini, licha ya kuondoka Nou Camp miaka miwili iliyopita staa huyo wa Inter Miami bado anaipenda Barcelona kutoka moyoni.
Akizungumza kwenye mahojiano na mchekeshaji maarufu kutoka Argentina Migue Granados, Messi alifafanua kuhusu tattoo hiyo.
“Nilichora tattoo kuonyesha mapenzi yangu kwa Barcelona. Ilikuwa kila kitu kwangu, ilichorwa vizuri sana, imechorwa mpira, nembo ya Barcelona, Argentina, na namba 10,” alisema Messi akaeleza alidizaini tattoo hiyo ili kubadilisha tattoo yake ya zamani aliyochora kwani alikuwa haipendi: “Sikuipenda tattoo ya zamani. Nilichora bila ya kufirikia. Sikuwa na wazo lolote, ndio maana nikabadilisha.”
Messi aligoma kurejea Barcelona licha ya familia yake kuonyesha nia lakini ilishindikana kutokana hali mbaya ya uchumi inayoendelea kuitafuna. Aliamua kutimkia Marekani licha ya kuwekewa ofa nono mezani na Al-Hilal.
Kwa upande wa Barcelona ilikuwa na imani ingemudu kumlipa Messi mshahara wa Dola 27 lakini ikashindikana, kwa sababu ilivunja sheria za kanuni za matumizi mabaya ya fedha iliyosababisha baadhi ya wachezaji wao kupuguza mishahara yao.