Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gyokeres kachagua timu

Muktasari:

  • Fowadi huyo, 26, amezivutia klabu nyingi baada ya kuonyesha kiwango huko Sporting Lisbon tangu alipojiunga mwaka 2023 akitokea Coventry, akifunga mabao 95 katika mechi 99 alizochezea miamba hiyo ya soka ya Ureno.

LISBON, URENO: STRAIKA, Viktor Gyokeres ameshafanya uamuzi wa kutua kwenye Ligi Kuu England na tayari ameshachagua klabu yake mpya ya kwenda kuitumikia msimu ujao.

Fowadi huyo, 26, amezivutia klabu nyingi baada ya kuonyesha kiwango huko Sporting Lisbon tangu alipojiunga mwaka 2023 akitokea Coventry, akifunga mabao 95 katika mechi 99 alizochezea miamba hiyo ya soka ya Ureno.

Arsenal na Manchester United zimekuwa zikisaka mshambuliaji wa kuwafungia mabao.

Gyokeres amekuwa akitajwa kuwa moja ya aina ya washambuliaji hao, ambao kwenye mkataba wake kumeripotiwa kuwekwa kipengele kinachohitaji kulipwa Pauni 85 milioni kunasa huduma yake.

Lakini, kwa maelezo ya sasa, Sporting ipo tayari kupokea ofa ya Pauni 58 milioni.

Kwa mujibu wa talkSPORT, Arsenal ndio wapo kwenye mstari wa mbele ya kukamilisha dili hilo. Klabu hiyo ya London kaskazini imejipanga kufanya matumizi makubwa kwenye usajili wa dirisha lijalo ikihitaji kuandaa kikosi cha ubingwa baada ya msimu huu kumalizika patufu, huku straika ikiwa ni tatizo lao.

Kai Havertz alichezeshwa kwenye eneo hilo msimu huu, lakini baada ya kuumia na kulazimika kufanyiwa upasuaji, Arsenal imejikuta kwenye wakati mgumu na kulazimika kumtumia kiungo Mikel Merino kwenye eneo hilo, kwa sababu straika Gabriel Jesus naye ni mgonjwa.

Gyokeres yupo kwenye mchakato wa kuwa mchezaji wa kwanza wa kutoka nje ya Ligi Kuu tano bora za Ulaya kushinda Kiatu cha Dhahabu cha Ulaya baada ya miaka 23, hivyo Arsenal itakuwa imenasa mtambo wa mabao endapo itanasa saini yake.

Man United yenyewe inasaka straika pia baada ya msimu huu kufunga mabao 42 tu Ligi Kuu Englad, huku washambuliaji Rasmud Hojlund na Joshua Zirkzee wakishindwa kumaliza kiu ya mabao. Faida ya Man United ni Ruben Amorim, ambaye alikuwa akimnoa Gyokeres Sporting.

Kushuka kwa bei ya Gyokeres itafutia klabu nyingi hasa baada ya Newcastle United kung’ang’ania kulipwa Pauni 150 milioni kwa timu zinazomtaka straika wao Alexander Isak baada ya kufunga mabao 23 kwenye ligi msimu huu.