Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Siri ya kilio cha baba yake EndricK ni hii

Muktasari:

  • Inaelezwa kulikuwa na jumla ya mashabiki 43,000 katika dimba la Santiago Bernabeu waliofika kumuona mchezaji huyo akitambulishwa mbele yao akiwa na jezi ya timu hiyo.

MADRID, HISPANIA: WIKIENDI iliyopita, kinda kutoka Brazil, Endrick alitambulishwa kwa mashabiki kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu ikiwa ni siku chache tu tangu akamilishe usajili wake wa kujiunga na mabingwa hao wa Ulaya akitokea Palmeiras.

Inaelezwa kulikuwa na jumla ya mashabiki 43,000 katika dimba la Santiago Bernabeu waliofika kumuona mchezaji huyo akitambulishwa mbele yao akiwa na jezi ya timu hiyo.

Wakati staa huyu anatambulishwa, uwanjani hapo pia kulikuwa na familia yake ikiongozwa na baba yake Doulgas aliyekuwa akilia muda wote.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari, Fabrizo Romano kilichokuwa kinamliza baba huyo ni historia ya maisha duni waliyopitia kabla ya mtoto wake kufiki hatua hiyo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Fabrizo aliandika kwamba Douglas alisema: “Bado nakumbuka, siku moja wakati huo Endrick alikuwa bado mtoto mdogo, alikuja kwangu na kuniambia, baba nina njaa sana naomba kitu cha kula. Nilikuwa katika sofa nikajaribu kuangalia katika kabati na friji sikuona kitu chochote cha kumpa, nikamwambia mwanangu Endrick sina kitu cha kukupa kisha nikaanza kumwaga machozi, Endrick akaja, akanikumbatia kwa muda mrefu kisha akaniambia, baba usilie, mimi nitakuwa  mchezaji mpira ni nitakutoa katika huu umasikini.”

Endrick mwenye umri wa miaka 18, katika utambulisho wake aliwashukuru mashabiki kwa lugha ya Kihispania kisha akaelezea safari yake kutoka Brazil hadi Madrid na wakati anaongea hayo macho yake yalikuwa wakitokwa na machozi.

Endrick aliwaambia mashabiki kuwa ilikuwa ndoto ya maisha yake kuichezea Madrid.

“Nina furaha sana. Tangu nikiwa mtoto nimekuwa shabiki wa Madrid na sasa naenda kuichezea Madrid.

“Nipo hapa, nitacheza, nina furaha sana, familia yangu pia ina furaha. Sina maneno ambayo yataelezea vile ninavyojisikia, siku zote nilikuwa natamani kuwa hapa na kuichezea Madrid, leo ndoto imetimia, sitasema uongo sikutarajia wingi huu wa watu.”

Endrick ambaye anacheza kama straika, alisajiliwa na Madrid, Desemba 2022, lakini hakuweza kujiunga na timu kwa sababu bado hakuwa ametimiza umri wa miaka 18.

Anakadiriwa kuigharimu Madrid kiasi cha Pauni 29.5 milioni na pesa hiyo inaweza ikaongezeka zaidi kutokana na kiwango atakachoonyesha, Palmeiras yenyewe imeutaja usajili huo kama ghali zaidi katika historia ya soka la Brazil hadi sasa, hiyo ikiwa na mjumuisho wa wachezaji walionunuliwa kutokea nchini humo kwenda Ulaya.