Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hispania yalipiza kisasi ikitinga fainali ya Kombe la Dunia

Muktasari:

  • Mechi hiyo iliyopigwa Uwanja wa Dallas nchini Marekani, imefuta kumbukumbu mbaya ya Hispania ilipoondolewa kwenye hatua ya 16 bora mwaka 2006, hivyo imelipa kisasi cha miaka 20 iliyopita.

DALLAS, MAREKANI: HATIMAYE kisasi kimelipwa! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Hispania kuitandika Ufaransa mabao 2-0 na kutinga hatua ya fainali ya Kombe la Dunia 2026.

Mechi hiyo iliyopigwa Uwanja wa Dallas nchini Marekani, imefuta kumbukumbu mbaya ya Hispania ilipoondolewa kwenye hatua ya 16 bora mwaka 2006, hivyo imelipa kisasi cha miaka 20 iliyopita.

Mara ya mwisho mataifa hayo yalipokutana kwenye Kombe la Dunia, ilikuwa Juni 27, 2006 nchini Ujerumani, ambapo Ufaransa ya nahodha Zinedine Zidane iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 katika hatua ya 16 Bora na kuzima ndoto za Hispania kusonga mbele.

Lakini safari hii kikosi cha Luis de la Fuente, kimeonyesha ukomavu mkubwa na kuondoka na ushindi uliokifanya kifike hatua ya fainali ya mashindano hayo.

Hispania ilianza mchezo kwa kasi na kuonyesha mapema kwamba haikuwa tayari kurudia makosa ya miaka 20 iliyopita.

Lamine Yamal aliendelea kuwa tishio upande wa kulia wa Hispania, akiwalazimisha mabeki wa Ufaransa kufanya makosa mara kwa mara. Presha hiyo ilizaa matunda dakika ya 22 baada ya Lucas Digne kumfanyia madhambi Yamal ndani ya eneo la hatari na mwamuzi kuamuru penalti ambayo ilipigwa na Mikel Oyarzabal na kuandika bao la kwanza.

Bao hilo liliifanya Hispania kucheza kwa kujiamini zaidi huku ikidhibiti kasi ya mchezo na kuwalazimisha Wafaransa kukimbizana na mpira.

Takwimu za kipindi cha kwanza zilionyesha ubora wa Hispania licha ya timu zote mbili kugusa mpira mara nane ndani ya eneo la hatari la mpinzani.

Ufaransa ilijikuta kwenye wakati mgumu zaidi baada ya beki wake William Saliba kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo mapema kipindi cha kwanza, hali iliyomlazimu kocha kufanya mabadiliko ya mapema.

Pamoja na kuwa na nyota kama Kylian Mbappé, Wafaransa walishindwa kupata mwanya wa kuivunja safu ya ulinzi wa Hispania iliyokuwa imara kuanzia kwa walinzi hadi kipa.

Kipindi cha pili kilianza kwa Ufaransa kujaribu kufanya mashambulizi mengi zaidi, lakini kila walipofika mbele walikutana na ukuta wa mabeki wa Hispania.

La Roja iliendelea kucheza kwa utulivu, ikitumia pasi fupi fupi na kutawala sehemu kubwa ya kiungo.

Dakika ya 58, Hispania ilipata bao la pili kupitia kwa Pedro Porro aliyemalizia vizuri pasi ya Dani Olmo na kuifanya timu hiyo iongoze mabao 2-0.

Bao hilo lilizima kabisa matumaini ya Ufaransa ya kurejea mchezoni, huku Hispania ikicheza kwa kujiamini zaidi na kutawala mchezo.

Ufaransa iliongeza nguvu katika mashambulizi kwa kufanya mabadiliko kadhaa kwa kumuingiza Desire Doue, lakini haikupata njia ya kupenya safu ya ulinzi ya Hispania.

Mbappe leo hakuwa na madhara kwa safu ya ulinzi ya Hispania kwani alidhibitiwa vizuri katika kila jaribio alilokuwa akifanya.

Mechi nyingine ya nusu fainali itapigwa Jumatano ya Julai 15, 2026 ikiwakutanisha Argentina na England. Mshindi wa mechi hiyo atakakutana na Hispania katika fainali itakayopigwa Julai 19, 2026, huku Ufaransa ikisubiri kucheza mechi ya kusaka nafasi ya tatu.