Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simeone, Ben White ‘wazinguana’, kisa nembo ya Atletico Madrid

SIMIONE Pict (1)

Muktasari:

  • Tukio hilo lilizuka baada ya filimbi ya mwisho, ambapo Ben White alionekana akikatiza moja kwa moja juu ya nembo ya klabu ya Atletico Madrid iliyochorwa uwanjani wakati akielekea kwenye chumba cha kubadilishia nguo.

MADRID, HISPANIA: KOCHA wa Atletico Madrid, Diego Simeone, amegonga vichwa vya habari baada ya kukabiliana vikali na beki wa Arsenal, Ben White, kufuatia sare ya 1-1 katika mechi ya mkondo wa kwanza ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (Uefa Champions League).

Tukio hilo lilizuka baada ya filimbi ya mwisho, ambapo Ben White alionekana akikatiza moja kwa moja juu ya nembo ya klabu ya Atletico Madrid iliyochorwa uwanjani wakati akielekea kwenye chumba cha kubadilishia nguo.

Nchini Hispania, nembo za klabu zilizopo uwanjani huchukuliwa kama vitu ‘takatifu’ na ni ishara ya heshima kubwa kwa wachezaji kuzunguka pembeni badala ya kuzikanyaga. 

NEM 01

Video zilizosambazwa na gazeti la Marca zinaonyesha wachezaji wengine wa Arsenal kama William Saliba na Martin Zubimendi wakizunguka pembeni ya nembo hiyo, lakini White aliamua kupita juu yake.

Kitendo hicho kilimkasirisha kwanza mtoto wa Simeone, Giuliano, kabla ya baba yake (Diego) kuingilia kati. Simeone alionekana akimpiga Ben White mgongoni mara kadhaa, akimshika mkono na kumsukuma kidogo, hali iliyozua malumbano ya maneno kabla ya walinzi kuingilia kati.

Mchezo huo ulikuwa na upinzani mkali ambapo mabao yote yalifungwa kwa njia ya penalti. Viktor Gyokeres aliitanguliza Arsenal kabla ya Julian Alvarez kuisawazishia Atletico baada ya Ben White kunawa mpira eneo la hatari.

NEM 02

Hata hivyo, ‘kivumbi’ kikubwa kilitokea baada ya mwamuzi kufuta penalti ya pili ya Arsenal kufuatia David Hancko kumfanyia madhambi Eberechi Eze. 

Baada ya shinikizo kubwa kutoka kwa Simeone na mashabiki wa nyumbani, mwamuzi alikwenda kwenye VAR na kubatilisha uamuzi wake, jambo lililomkasirisha sana kocha wa Arsenal, Mikel Arteta.

Akizungumza baada ya mechi hiyo, Arteta hakuficha hasira zake kuhusu uamuzi wa mwamuzi huyo.

NEM 03

"Inasikitisha sana. Kulikuwa na mguso wa wazi, mwamuzi ametoa uamuzi na huwezi kuubadilisha baada ya kuangalia marudio mara 13. Ni uamuzi mbaya na unabadilisha mwelekeo wa mchezo huu," amesema Arteta.

Licha ya sare hiyo na vurugu za nje ya uwanja, Arteta anaamini kikosi chake kiko kwenye nafasi nzuri.

"Tupo kwenye nafasi nzuri sana. Tunapaswa kucheza mbele ya mashabiki wetu (Emirates). Kila kitu kipo mikononi mwetu," amesema.