Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ligi ya Mabingwa Ulaya… Kinawaka

KINAWAKA Pict

Muktasari:

  • Chelsea ambayo imepoteza mechi mbili mfululizo za Ligi Kuu England mfululizo itakuwa inajipanga ili kushinda mechi yake ya kwanza ya michuano hiyo baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Bayern Munich kwa mabao 3-1 katika mashindano hayo.

LONDON, ENGLAND: LIGI ya Mabingwa Ulaya inaendelea leo kwa mechi tisa kupigwa ambapo vigogo wa Hispania Real Madrid, Chelsea, Bayern Munich, Liverpool, Inter Milan na Tottenham Hotspur watakuwa katika harakati za kuendelea kukusanya pointi ili kusogea kwenye nafasi za juu mapema.

Chelsea ambayo imepoteza mechi mbili mfululizo za Ligi Kuu England mfululizo itakuwa inajipanga ili kushinda mechi yake ya kwanza ya michuano hiyo baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Bayern Munich kwa mabao 3-1 katika mashindano hayo.

Mabingwa hao watetezi wa michuano ya Kombe la Dunia la Klabu watakutana na Benfica ambayo ipo chini ya kocha mpya Jose Mourinho aliyechukua mikoba ya kuinoa hivi karibuni. Mechi hiyo itapigwa kuanzia saa 4:00 usiku.

Liverpool iliyopata ushindi katika dakika za jioni dhidi ya Atletico Madrid kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Anfield leo itakuwa Uturuki kuvaana na mabingwa wa nchi hiyo, Galatasaray katika mechi ambayo itaanza pia saa 4:00 usiku.

KINA 01

Rekodi zinaonyesha katika mechi nne ambazo Liverpool ilicheza dhidi ya Galatasaray kuanzia 2002 imeshinda mara moja pekee, mbili zikimalizika kwa sare kisha moja ikipoteza.

Wana fainali wa michuano hiyo msimu uliopita, Inter Milan ambao msimu huu wana hali mbaya katika Ligi Kuu Italia wakiwa wameshapoteza mechi mbili kati ya tano watakuwa nyumbani kuikaribisha Slavia Praha ya Jamhuri ya Czechoslovakia.

Real Madrid imesafiri safari ndefu ya zaidi ya saa 10 kwenda Kazakhstan kwa ajili ya kuvaana na Kairat na mechi hiyo ndiyo itakuwa ya mapema zaidi kwa kesho ikitarajiwa kuanza saa 1:49 usiku.

KINA 02

Bayern Munich ambayo mechi ya kwanza ya michuano hiyo iliichapa Chelsea  3-1 ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani na sasa itaumana na Pafos ya huko Cyprus.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa upande mmoja, lakini katika soka lolote linaweza kutokea kwani katika mechi za karibuni wababe hao wa Bundesliga wamekuwa moto katika siku za karibuni kwenye mashindano ya ndani na Ulaya.

KINA 03

Atletico Madrid ya Diego Simione itakuwa na nafasi ya kurekebisha makosa yao ya kupoteza mechi ya kwanza itakapokutana na Eintracht Frankfurt ya Ujerumani.

Mechi zote zinatarajiwa kuanza saa 4:00 usiku isipokuwa ile ya Atalanta dhidi ya Club Brugge pamoja na ile ya Real Madrid itakayokipiga na Kairat.