Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simeone afunguka sababu ya kumvaa shabiki

CHOLO Pict

Muktasari:

  • Simeone aliona kikosi chake kikirejea mchezoni baada ya kuwa nyuma kwa mabao 2-0 na kukaribia kupata alama muhimu katika ligi hiyo.

LIVERPOOL, ENGLAND: KOCHA wa Atletico Madrid, Diego Simeone amefichua kwa nini aligombana na shabiki wa Liverpool baada ya Atletico Madrid kupoteza Anfield katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya juzi, Jumatano.

Simeone aliona kikosi chake kikirejea mchezoni baada ya kuwa nyuma kwa mabao 2-0 na kukaribia kupata alama muhimu katika ligi hiyo.

Hata hivyo, matumaini ya Atletico yalizimwa dakika za nyongeza baada ya Virgil van Dijk kufunga kwa kichwa na kuipa Liverpool ushindi wa mabao 3-2.

Baada ya bao hilo, Simeone alikasirika na kupelekwa nje ya uwanja baada ya kutaka kumkabili shabiki wa Liverpool aliyekuwapo jukwaani mara baada ya Van Dijk kufunga na walinzi wa uwanja walilazimika kumzuia kabla hajasukumwa kurudi nyuma.

Simeone pia alikimbilia kwa mwamuzi akilalamika kuhusu tukio hilo, jambo lililosababisha kutolewa kwa kadi nyekundu.

Haijulikani ni nini hasa kilichochochea hadi kuzuka kwa ugomvi huo, lakini Simeone alisema alilazimika kuvumilia 'matusi' kwa muda mrefu wa mchezo huo lakini mwishowe uvumilivu ulimshinda.

"Watu siku zote huzungumzia heshima, lakini mashabiki wanaweza kukutukana kutoka jukwaani muda wote wa mchezo. Siwezi kujibu chochote kwa sababu mimi ndiye kocha. Nilichokifanya hakina uhalali wowote, lakini ilikuwa ni lazima nifanye vile baada ya dakika 90 za matusi. Mwamuzi aliniambia anaelewa hali hiyo. Natumai Liverpool watajirekebisha upande huu na wakimtambua mhusika, aadhibiwe."

Alipoulizwa zaidi kuhusu matusi hayo, aliongeza:

"Nilikuwa napokea matusi muda wote wa mchezo. Na ishara chafu pia. Hawajui ni kitu gani mtu unapitia kwa wakati huo, lakini mimi ndiye nahitajika kubaki mtulivu, nivumilie matusi katika hali yoyote. Kwa nini? Kwa sababu niko kwenye nafasi ambayo nalazimika kuvumilia."

Kuhusu matokeo alisema: "Hatukuwa na bahati katika bao la kwanza; lilitutoa mchezoni, lakini kwa kujitoa na ubora wa wachezaji wangu tulirejea mchezoni. Tulikuwa tumeshikilia mchezo hadi bao zuri la Virgil lilipotuacha na uchungu, lakini bado tuna moyo wa kupambana."