Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba kazi ndo imeanza, Cadena apongeza usajili

Muktasari:

  • Kikosi hicho cha Simba kitakuwa nchini humo kwa muda wa siku zisizopungua 20 kujiandaa na msimu mpya.

KAZI ndio imeanza sasa katika kambi ya Simba iliyopo Ismailia, Misri. Ikiingia siku ya tano tangu kuanza kujifua kambini, mastaa wa Simba sasa ndio wameanza kazi chini ya kocha Fadlu Davids na wasaidizi wake.

Kikosi hicho cha Simba kitakuwa nchini humo kwa muda wa siku zisizopungua 20 kujiandaa na msimu mpya.

Licha ya kwamba kambi hiyo ilianza siku nne zilizopita lakini juzi Alhamisi ndio kazi imeanza rasmi baada ya kikosi kamili kukamilika ikiwa ni baada ya kuanza kazi kwa kocha mkuu Fadlus, msaidizi Darian Wilken, wa makipa Wayne Sandlands, wa viungo Riedoh Berdien na mtathimini michezo, Mueez Kajee waliochelewa Dar es Salaam sambamba na Selemani Matola aliyetangulia na timu na kuianzisha kambi hiyo iliyopo kwenye hoteli ya kifahari ya Mercure Ismailia Forsan Islands.

Kazi hiyo ni ya kimkakati kutokana na muda uliopo kwani timu hiyo itarejea nchini kabla ya Agosti Mosi kwa maandalizi ya tamasha la Simba Day litakalofanyika Agosti 3, ikiwa ni utambulisho wa kikosi rasmi kwa ajili ya msimu ujao.

Mara baada ya kutua kambini, inaelezwa Fadlu alizungumza na wachezaji kisha kuanza kuwapigisha tizi, wakianza wasaidizi wake, kisha yeye kuhamia na ubao mahususi wa kufundishia kuonyesha kwamba kocha huyo yupo siriazi na hadi timu itakapoondoka Ismailia, huenda mambo yakawa moto kwa Wekundu hao.

Awali, baada ya Matola kuwapigisha tizi la kutafuta pumzi na stamina kwa kukimbia zaidi na kujifua gym, ujio wa makocha hao wapya wamefanya mazoezi hayo kuhamia zaidi uwanjani na wachezaji kuanza kugusa mpira wakiwa na mbinu za kiufundi, huku boli likichezwa kwa pasi nyingi na kasi.

Moja ya viongozi wa Simba aliyepo na timu huko Misri, ameliambia Mwanaspoti benchi la ufundi limesisitiza kwenda na muda ili kila kitu kiwe vizuri huku akiweka wazi ratiba ya mazoezi ya Wekundu hao wa Msimbazi ambao wamesafisha karibu kikosi kizima cha msimu uliopita na kusajili machine mpya zisizopungua 12.

"Sisi tunachokifanya ni kuratibu tu, lakini kazi kubwa itafanywa na benchi la ufundi na tayari tumeongea nao na wametutaka kujali sana muda," alisema kiongozi huyo aliyeomba kuhifadhiwa jina na kuongeza;

"Kwa taarifa tuliyonayo sasa timu itamalizia wiki hii kwa mazoezi mepesi na yale ya utimamu wa mwili kisha wiki ijayo ndipo mbinu na mambo mengine ya kiufundi yataanza kufanyika. Tunatakiwa Agosti Mosi, tuwe Tanzania lakini kabla ya hapo tunaamini benchi la ufundi chini ya Fadlu litakuwa limemaliza kazi yake kwa kiasi kikubwa kwani katika wiki ya mwisho tukiwa hapa Ismailia tutacheza mechi mbili hadi tatu za kirafiki ili kupima maandalizi yetu."

Katika muda huo, Fadlu na wasaidizi wake ufundi watakuwa wakijenga timu yenye maelewano ndani na nje ya uwaja, morali ya juu na kufundisha mifumo na mbinu ambazo chama hilo la Msimbazi litakuwa likitumia.

Ni kama mwanzo mpya kwani katika kikosi hicho cha Simba kuna wachezaji wapya 14 wa maeneo tofauti ambao ni mabeki Abdulrazak Hamza, Kelvin Kijiri, Valentin Nouma na Chamou Karaboue.

Viungo ni Debora Fernandes, Agustine Okejepha, Omary Omary, Charles Ahoua, Yusuph Kagoma, Awesu Awesu na Joshua Mutale huku washambuliaji wakiwa Valentino Mashaka na Steven Mukwala.

Waliokuwepo kikosini kwa msimu uliopita na wamesalia ni makipa Ayoub Lakred, Hussein Abel, Ally Salim na Ahmed Feruz, mabeki Che Malone Fondoh, Mohamed Hussein 'Tshabalala', Shomari Kapombe, Hussein Kazi na David Kameta 'Duchu'.

Viungo ni Fabrice Ngoma, Mzamiru Yassin na Kibu Denis huku mshambuliaji akiwa Freddy Michael pekee.


WASIKIE WADAU

Kocha wa zamani wa Yanga na mchambuzi wa soka, Kennedy Mwaisabula 'Mzazi' alisema 'pre-season' ni eneo ambalo timu inajengwa na inahitaji kuwa na muda wa wiki moja hadi sita.

"Ni kipindi ambacho timu inajengwa kwani wachezaji wengi wanakuwa wapya lakini hata waliokuwapo wanakuwa wametoka mapumziko. Ni wakati wa kujenga kila kitu na kuanza upya kabisa hivyo timu inatakiwa kupata muda wa kutosha ili kukamilisha kila kitu kwa ubora kabla ya msimu kuanza," alisema Mwaisabula.

Aliyekuwa kocha wa makipa wa Simba, Dani Cadena aliipongeza timu hiyo kwa kusajili wachezaji wapya na kufanya kambi iwe nje ya nchi huku akitaja sababu za kiufundi.

"Unapoitoa timu kwenye eneo lake na kuipeleka nje unaongeza utulivu kwa wachezaji lakini pia unawafanya waone thamani yao na ukubwa wa timu.

Nawapongeza Simba kwa hili na nawatakia mema katika maandalizi ya msimu ujao," alisema Cadena.

Ofisa habari wa Simba, Ahmed Ally alisema timu hiyo kwa sasa imekamilika na kinachofuata ni kusuka kikosi imara kwa msimu ujao.

"Tumefanya usajili wa maana kulingana na matakwa ya kikosi chetu na tumekamilisha kila kitu. Kwa sasa tunasuka mipango na mikakati itakayotufanya tuwe bora zaidi uwanjani na kutoa burudani kwa mashabiki zetu," alisema Ahmed.