Shearer aiponda beki Man City
Muktasari:
- Jumamosi usiku, City ilikubali kichapo cha mabao 2-1 ugenini kwenye Uwanja wa St James’ Park na kupoteza pointi tatu muhimu ambazo zingeifanya iikaribie vinara Arsenal ambayo ilishinda mabao 4-1 dhidi ya Tottenham juzi usiku na hivyo kuachwa kwa tofauti ya pointi sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.
NEWCASTEL, ENGLAND: GWIJI wa zamani wa Newcastle United, Alan Shearer ameionya beki ya Manchester City inaweza ikaharibu matumaini ya miamba hiyo kutwaa taji la Ligi Kuu England.
Jumamosi usiku, City ilikubali kichapo cha mabao 2-1 ugenini kwenye Uwanja wa St James’ Park na kupoteza pointi tatu muhimu ambazo zingeifanya iikaribie vinara Arsenal ambayo ilishinda mabao 4-1 dhidi ya Tottenham juzi usiku na hivyo kuachwa kwa tofauti ya pointi sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.
City inayonolewa na Pep Guardiola aliyetua kikosini hapo tangu msimu wa 2016/17, ametawala soka la England akiipa miamba hiyo mataji manne mfululizo kabla ya kuporomoka ghafla msimu uliopita na Liverpool kubeba na sasa inataka kurudisha utawala wake.
City inaonekana kuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kuipa changamoto Arsenal kileleni, lakini kupoteza mechi hiyo kumeipa Arsenal nafasi ya kuzidi kuiacha katika mchakamchaka huo, ingawa bado haijaondolewa kwenye mbio hizo.
“Hakika hawako vizuri kama walivyokuwa na huenda tusije tukawaona tena wakifikia kiwango kile walichowahi kuwa nacho,” Shearer alisema na kuongeza;
“Namaanisha kiwango cha ushindani katika kushinda mataji, kufunga mabao na mambo yote hayo, walichokuwa nacho, sina uhakika kama wataweza kufikia hapo tena.
“Wasiwasi wangu ni kwenye safu ya beki. Daima watapata mabao, hasa wakiwa na Haaland mbele, lakini beki haiko makini kama walivyokuwa.”