Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pep Guardiola, Bruno Guimaraes wazinguana

PEP Pict

Muktasari:

  • Kocha huyo wa Man City, 54, alionekana mwenye hasira kiasi cha kuingiza katika majibizano hayo mara baada ya mechi kumalizika.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola aliingia katika majibizano na staa wa Newcastle, Bruno Guimaraes, maofisa wa mechi na mpigapicha baada ya timu yake kupoteza kwa mabao 2-1 katika mechi iliyopigwa Uwanja wa St James’ Park.

Kocha huyo wa Man City, 54, alionekana mwenye hasira kiasi cha kuingiza katika majibizano hayo mara baada ya mechi kumalizika.

Mechi hiyo ilijaa utata uliosababishwa na baadhi ya matukio na Guardiola alikasirishwa na kutopewa penalti kipindi cha kwanza wakati Phil Foden alipochezewa vibaya na Fabian Schar.

Kulikuwa pia na tukio lililoonyesha huenda kipa wa Man City Gianluigi Donnarumma alifanyiwa faulo kabla ya Newcastle kufunga bao lapili, pia ilitajwa aliyehusika katika bao hilo alikuwa katika eneo la kuotea.

Licha ya Man City kuhisi imeonewa, bao hilo lilikubalika na hilo ndio lilimpa hasira Guardiola ambaye baada ya mechi, alianza kujibizana na Guimaraes kabla ya kuzungumza na mwamuzi Sam Barott na wasaidizi wake.

Alipoulizwa na BBC kuhusu matukio hayo baada ya mechi Guardiola amesema: “Hakuna maswali, kila kitu kiko sawa.”

Wakati huo huo alipokwenda kuzungumza na Sky Sports kuhusu mazungumzo yake na Guimaraes, Guardiola amesema: “Nilimwambia ni mchezaji mzuri sana lakini mazungumzo hayo yalikuwa ni binafsi.”

Mabao mawili ya Barnes yalikuwa pigo kubwa kwa Man City, ambayo ilikuwa na matumaini ya kuendelea kupunguza pengo la alama kati yao na vinara Arsenal.