Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sakata la kesi 115 za Man City linavyosubiriwa

MAN CITY Pict

Muktasari:

  • Man City ilifunguliwa mashtaka mwanzoni mwa mwaka 2023 ikidaiwa kukiuka utaratibu na kanuni za matumizi ya pesa kwenye soka kwa kipindi cha muda mrefu.

LONDON, ENGLAND: MANCHSTER City na klabu nyingine za Ligi Kuu England zinasubiri kwa hamu hukumu ya kesi inayoikabili miamba hiyo inayonolewa na Mhispaniola Pep Guardiola juu ya udanganyifu kwenye matumizi ya pesa.

Man City ilifunguliwa mashtaka mwanzoni mwa mwaka 2023 ikidaiwa kukiuka utaratibu na kanuni za matumizi ya pesa kwenye soka kwa kipindi cha muda mrefu.

Man City imekanusha kufanya makosa hayo, huku kamati huru ikipewa kazi hiyo ya kufanya uchanguzi juu ya kesi hiyo kwa muda sasa ikisubiriwa hukumu. Man City inakabiliwa na mashtaka 115 ya kudaiwa kufanya udanganyifu juu ya matumizi kwenye klabu hiyo.


MAN 01

Kosa lilifanywa lini?

Ligi Kuu England ilibainisha kwenye ripoti yake ya Februari 6, 2023 imelezea madai hayo ya Man City kukiuka kanuni za matumizi kwenye kamati. Man City ilidai kwamba imetoa taarifa zote muhimu za kuhusu matumizi yao ya pesa na kwamba hakukuwa na udanganyifu wowote. Ligi Kuu England ilibainisha kwamba haiwezi kufanya malumbano yoyote kwenye jambo hilo na kinachosubiriwa ni majibu ya kamati maalumu iliyopewa jukumu hilo ili kutambua kama kuna kosa limetendeka au la.


MAN 02

Kipi wanachoshtakiwa?

Msingi mkubwa wa mashtaka yanayoikabili Man City ni kukiuka kanuni za matumizi juu ya taarifa zao za kifedha, hazikuwa zikiweka kwa uwazi juu ya malipo kwa wachezaji na makocha juu ya mishahara yao. Man City inakabiliwa pia na mashtaka ya kushindwa kutoa ushirikiano wakati wa uchunguzi wa kukiuka kanuni za matumizi kwenye Ligi Kuu England na taratibu za Uefa. Man City ilishindwa kutoa taarifa sasa fedha mara 54 kuanzia msimu wa 2009/10 hadi 2017/18. Man City ilishindwa kutoa ushirikiano kwa wachunguzi wa Ligi Kuu England mara 35 kuanzia Desemba 2018 hadi Februari 2023.

Man City ilishindwa mara 14 kutoa taarifa sahihi ya kuhusu malipo ya wachezaji na makocha waliyofanya kuanzia 2009/10 hadi 2017/18. Man City imekiuka mara saba juu ya PSR kuanzia msimu wa 2015/16 hadi 2017/18. Man City imeshindwa mara tano kwenda sambamba na sheria za Uefa ikiwamo club licensing na financial fair play (FFP) kuanzia 2013/14 hadi 2017/18.


MAN 03

Adhabu gani inaikabili Man City?

Hakuna adhabu moja ambayo inaweza kuikumba Man City endapo kama itakutwa na hatia, lakini miongoni mwa adhabu hizo zipo kali zaidi.

Ukiweka kando suala la kupokwa pointi kama ilivyotokea kwa timu za Everton na Nottingham Forest zilipokiuka kanuni ya PSR. Ligi Kuu England inaweza kuiadhibu Man United kutofanya usajili na kuwapoka mataji. Kuondolewa kwenye Ligi Kuu England pia kunaweza kuwa moja ya adhabu zinazoweza kuikabili Man City.

Guardiola alizungumzia hilo la kuondolewa kwenye ligi, Novemba 2023 aliposema: “Bila shaka nitafikiria juu ya hatima yangu kama hilo litategemea kama tutakuwa kwenye Ligi Kuu England au League One. Ni wazi kuna nafasi kubwa ya kubaki kama tutakuwa kwenye League One kuliko kama tutakuwa kwenye Ligi Kuu England.”


MAN 04

Ligi Kuu England inasemaje?

Kwa kifupi, bosi mkubwa wa Ligi Kuu England alisema hawezi kusema kitu chochote kwa sasa kwenye hadhara hadi hapo hukumu ya mwisho itakapotolewa endapo kama kutakuwa na makosa yaliyofanyika ambayo yanakinzana na sheria zake.

Taarifa ya Ligi Kuu England ilibainisha: “Tunachofanya ni kuchapisha mashtaka yakibainishwa na tutachapisha hukumu itakayotolewa. Hilo lipo kati ya kamati huru na inafanya jambo hilo kwa usiri mkubwa.”


Kwanini hukumu inachukua muda mrefu?

Urefu wa sakata hilo unatokana na ukubwa wa kesi yenyewe. Kwa mujibu wa The i Paper imepitia nakala 250,000 za kesi hiyo. Kesi hiyo ilisikilizwa kwa wiki 12 ikiwa ni muda mrefu tofauti na siku tano ambazo zilitumika kwa Everton kumaliza kesi yake ya PSR. Lakini, kesi ya Man City inazidi mwaka sasa. Uamuzi wowote utakaofikiwa basi utahusisha ripoti yenye mamia ya kurasa.