Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cole Palmer adaiwa kuchoshwa Chelsea

PALMER Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo wa kimataifa wa England, 23, anaripotiwa kuvutia vigogo kadhaa wa Ulaya, huku Manchester United ikitajwa kuwa moja ya klabu zinazomwania kwa nguvu.

LONDON, ENGLAND: KIUNGO mshambuliaji wa Chelsea, Cole Palmer inadaiwa kuzidi kukata tamaa na maisha ndani ya klabu hiyo na sasa yupo tayari kuangalia uwezekano wa kuondoka Stamford Bridge dirisha hili la usajili.

Nyota huyo wa kimataifa wa England, 23, anaripotiwa kuvutia vigogo kadhaa wa Ulaya, huku Manchester United ikitajwa kuwa moja ya klabu zinazomwania kwa nguvu.

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali, Palmer hajafurahishwa na mabadiliko ya kiufundi yaliyofanywa na kocha Liam Rosenior, ambayo yanaelezwa kupunguza uhuru wake wa kucheza na kuathiri uwezo wake wa kuamua matokeo ya mechi kama alivyofanya msimu wake wa kwanza Chelsea.

Mbali na hilo, kuondoka kwa mshambuliaji Nicolas Jackson, aliyejiunga na Bayern Munich kwa mkopo wa msimu mzima, kumeelezwa kumechangia kutoridhishwa kwa Palmer kutokana na wawili hao kuwa na maelewano mazuri uwanjani.

PALM 01

Chelsea iliwasajili Joao Pedro na Liam Delap kuziba pengo hilo, lakini inadaiwa safu ya ushambuliaji ya timu hiyo bado haijafikia kiwango ilichokuwa nacho msimu uliopita.

Hali hiyo imeziweka Manchester United, Real Madrid na Bayern Munich katika nafasi ya kufuatilia kwa karibu mustakabali wa mchezaji huyo.

Licha ya Chelsea kumchukulia Palmer kama mchezaji asiyegusika na akiwa na mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo hadi mwaka 2033, taarifa zinaeleza thamani yake inaweza kufikia Pauni milioni 150.

Palmer, ambaye ni shabiki wa muda mrefu wa Manchester United, amekuwa akihusishwa mara kwa mara na uwezekano wa kuhamia Old Trafford.

PALM 02

Maslahi ya United yanaongezeka pia kutokana na uwepo wa mkurugenzi wa soka wa klabu hiyo, Jason Wilcox, ambaye aliwahi kufanya kazi katika akademi ya Manchester City wakati Palmer akipanda ngazi za maendeleo.

Wilcox anadaiwa kuwa mmoja wa watu wanaovutiwa zaidi na uwezo wa Palmer, huku akiungwa mkono na Ofisa Mtendaji Mkuu wa United, Omar Berrada, ambaye pia ana historia ya kufanya kazi Manchester City.

Msimu uliopita haukuwa rahisi kwa Palmer. Nyota huyo alionyesha wazi kutoridhishwa kwake katika mchezo dhidi ya Everton baada ya kuonekana akimlalamikia Pedro Neto baada ya kushindwa kumpa nafasi nzuri ya kufunga.

Licha ya kuonyesha dalili za kuchoshwa na hali ya sasa, vyanzo vya ndani ya Chelsea vinasisitiza Palmer bado ameendelea kujitoa kwa timu, ingawa kiwango chake kimeonekana kushuka.

Chelsea kwa sasa ipo nafasi ya sita katika Ligi Kuu England na inapambana kuhakikisha inafuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, jambo ambalo linaweza kuwa muhimu katika kumshawishi Palmer kuendelea kubaki Stamford Bridge.