Sevilla huko Europa ni balaa

Klabu ya Sevilla imeendeleza rekodi yake katika kombe la Europa baada ya kutwaa taji hilo kwa mara ya saba mfululizo.

Sevilla ambayo inashikilia nafasi ya 11 katika Ligi ya Spain (La Liga) imeshinda kombe hilo jana Jumatano Mei 31, 2023 kwa kuifunga AS Roma ya Italia kwa Penalti 4-1 kufuatia dakika 120' kumalizika kwa timu hizo kupata sare ya bao 1-1.

Bao la Roma lilifungwa na Paulo Dybala dakika ya 35' huku Sevilla ikipata mteremko baada ya Beki wa AS Roma, Gianluca Mancini kujifunga dakika 55'.

Ushindi wa Sevilla kwenye fainali hiyo umetia doa kwenye rekodi za Kocha wa AS Roma, José Mourinho kwani ni mara yake ya kwanza kupoteza mchezo wa fainali kwani hajawahi kupoteza mchezo wa fainali.

Hivyo katika mashindano ya Klabu Bingwa Ulaya, Sevilla imeshinda katika fainali ya Europa iliyochezwa mwaka 2005/06, 2006/07,  2013/14, 214/15, 2015/16 (UCL) 2019/20 na 2022/23.

Pamoja na Sevilla kushika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa LaLiga, kushinda Europa kunawafanya wafuzu kucheza Klabu Bingwa Ulaya (Uefa) moja kwa moja na kuifanya LaLiga kuwa na uwakilishi wa timu tano badala ya nne kwenye mashindano ya Uefa.