Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sesko kukosa mechi kibao Man United

SESKO Pict

Muktasari:

  • Sesko, 23, alilazimika kutoka uwanjani dakika 88 katika mechi ya sare ya 2-2 dhidi ya Tottenham Hotspur, Novemba 8, wakati kwenye mechi hiyo aliingia kwenye kipindi cha pili kutoka benchini.

MANCHESTER, ENGLAND: STRAIKA wa Manchester United, Benjamin Sesko huenda akawa nje ya uwanja kwa takriban mwezi kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya goti huku jambo hilo likimshuhudia akikosa mechi kibao zaidi ya sita.

Sesko, 23, alilazimika kutoka uwanjani dakika 88 katika mechi ya sare ya 2-2 dhidi ya Tottenham Hotspur, Novemba 8, wakati kwenye mechi hiyo aliingia kwenye kipindi cha pili kutoka benchini.

Sesko alijiondoa kwenye kikosi cha Slovenia katika mechi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Kosovo na Sweden, lakini uchunguzi wa awali wa Man United ulionyesha straika huyo hakuwa amepeta majeraha makubwa sana.

Kocha wa Man United, Ruben Amorim alimwanzishia benchini Sesko katika mechi dhidi ya Spurs, huku akimpanga Matheus Cunha kama Namba 9 wa uongo. Amorim alimweka benchi Sesko pia kwenye mechi ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Liverpool mwezi uliopita.

SES 02

Straika Sesko amefunga mabao mawili katika mechi 12 alizoichezea Man United tangu aliponaswa kwa ada ya Pauni 73.62 milioni kutoka RB Leipzig kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi. Kwenye kipindi cha usajili, Man United chaguo lake la kwanza kwenye msako wa mastraika, alikuwa Liam Delap, lakini staa huyo aliamua kuhamia Chelsea baada ya kulipa Pauni 30 milioni kuvunja mkataba wake huko Ipswich Town.

Straika Victor Gyokeres alichagua kwenda Arsenal na Aston Villa iliweka ngumu kwa Ollie Watkins, hivyo, Man United iliamua kwenda Leipzig kwenda kunasa saini ya Sesko, ambaye mwaka 2022 aligomea ishu ya kutua Old Trafford na kwenda kujiunga na RB Leipzig. Man United ilijaribu pia kutaka kumsajili straika Nicolas Jackson kutoka Chelsea.

SES 03

Lakini, kocha Ruben Amorim ametosheka na usajili wa safu yake ya ushambuliaji baada ya kumnasa Bryan Mbeumo. Staa huyo wa Cameroon ametua Old Trafford kuungana na Mbrazili, Matheus Cunha, aliyesajiliwa kutoka Wolves kwa ada ya Pauni 62.5 milioni.

Man United imeanza kuwa kwenye kiwango bora na sasa imecheza mechi tano kwenye Ligi Kuu England bila ya kupoteza, ikishinda tatu na kutoka sare mbili.


MECHI AMBAZO SESKO ATAKOSA MAN UNITED

-Novemba 24 vs Everton (nyumbani)

-Novemba 30 vs Crystal Palace (ugenini)

-Desemba 4 vs West Ham (nyumbani)

-Desemba 8 vs Wolves (ugenini)

-Desemba 15 vs Bournemouth (nyumbani)

-Desemba 21 vs Aston Villa (ugenini)