Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastraika wanne kumbadili Benjamin Sesko

SESKO Pict

Muktasari:

  • Straika huyo aliyesajiliwa kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi alitokea benchini kwenye mechi dhidi ya Tottenham Hotspur, Jumamosi iliyopita kabla ya kutoka nje kwa kushindwa kumaliza mechi na kuifanya timu yake kubaki na wachezaji 10 uwanjani kwa sababu kocha Ruben Amorim alikuwa ameshamaliza kufanya mabadiliko ya wachezaji wote.

MANCHESTER, ENGLAND: MAJERAHA ya straika Benjamin Sesko yanaiacha Manchester United njiapanda kwa wiki zijazo katika mchakamchaka wa kufanya vizuri kwenye mechi za Ligi Kuu England.

Straika huyo aliyesajiliwa kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi alitokea benchini kwenye mechi dhidi ya Tottenham Hotspur, Jumamosi iliyopita kabla ya kutoka nje kwa kushindwa kumaliza mechi na kuifanya timu yake kubaki na wachezaji 10 uwanjani kwa sababu kocha Ruben Amorim alikuwa ameshamaliza kufanya mabadiliko ya wachezaji wote.

Bado haifahamiki hali ya staa huyo itakavyokuwa baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa, lakini Man United bado ina kitu cha kufanya endapo kama tatizo la Sesko litakuwa kubwa.

Kocha Amorim aliamua kuanza na safu ya ushambuliaji ya Matheus Cunha, Bryan Mbeumo na Amad katika mechi hiyo ya Spurs na kuna muda alikuwa akimtumia Mason Mount kwenye fowadi. Mbeumo, kinara wa mabao wa Man United, si muda mrefu atakwenda kwenye fainali za Afcon, hivyo jambo hilo litamfanya kocha Amorim kuwa na upungufu kwenye fowadi yake.

Kutokana na hilo, Amorim, 40, alikiri kuna ulazima wa kufikiria dirisha la Januari.

“Tutaangalia kila kitu, tutaangalia nini kitatokea kwa Ben,” amesema Amorim.

“Tutakwenda kuwa na tatizo la Afcon, tushalifahamu hilo. Hivyo, unaweza kuona jinsi hali inavyokwenda kuwa ngumu. Lakini, tutaona dirisha litakapofunguliwa hali itakuwaje, kama tunaweza kufanya kitu basi tutaangalia kitakachotokea.”

Kama Man United itaingia sokoni dirisha la Januari, ni mastaa gani wa safu ya ushambuliaji inaweza kupambana kwenda kunasa saini zao.


SES 01

1. Dusan Vlahovic; Straika huyo wa kimataifa wa Serbia atakuwa mchezaji huru mwisho wa msimu, huku klabu nyingine kama Barcelona, Bayern Munich na Tottenham zitapambana kunasa huduma yake. Man United inaweza kuwahi kumnasa dirisha la Januari.


SES 02

2. Vitor Roque; Man United imeripotiwa kumsaka Vitor Roque kwa nguvu zote na huenda ikatoa Pauni 38 milioni kumnasa straika huyo wa Palmeiras. Fowadi huyo alifunga mabao 13 katika mechi 28 tangu aliporudi huko Brazil akitokea Barcelona.


SES 03

3. Ollie Watkins; Straika huyu hana wakati mzuri sana kwenye Ligi Kuu England msimu huu, akifunga mara moja tu katika mechi 11, lakini hilo halina maana ya kumweka kando kwenye orodha ya wachezaji ambao Man United inaweza kuwanasa dirisha la Januari kutokana na uzoefu wake.


SES 04

4. Endrick; Fowadi huyo wa Real Madrid, Endrick, 19, yupo kwenye uwezekano mkubwa wa kubadili timu kwenye dirisha la Januari. Lyon ya Ufaransa inapiga hesabu za kumnasa kwenye dirisha la majira ya baridi huko Ulaya, lakini Man United inaweza kuvamia na kunasa huduma yake hata kama ni kwa mkopo ili akakipige Old Trafford.