Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sergio Ramos kuinunua Sevilla

RAMOS Pict

Muktasari:

  • Gwiji huyo wa Hispania na Real Madrid yuko tayari kujiunga na mradi unaohusisha watu wenye nguvu kubwa, akitazama maisha yake baada ya uchezaji uwanjani.

MADRID, HISPANIA: BEKI wa boli, Sergio Ramos amepanga kurejea kwa kishindo katika ulimwengu wa soka na inaripotiwa kuwa anaweza kuinunua moja ya klabu alizowahi kuzichezea zamani.

Gwiji huyo wa Hispania na Real Madrid yuko tayari kujiunga na mradi unaohusisha watu wenye nguvu kubwa, akitazama maisha yake baada ya uchezaji uwanjani.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 39 aliichezea Monterrey mara ya mwisho na bado hajawa tayari kustaafu rasmi, akilenga kuendelea na safari yake ya soka iliyojaa mafanikio.

Beki huyo asiye na mzaha wowote ameshinda kila kitu katika ngazi ya klabu akiwa na Los Blancos nchini Hispania, na pia alishinda mataji ya ligi na kombe la ndani akiwa PSG.

Katika ngazi ya kimataifa, aliichezea Hispania mara 180, akitwaa Kombe la Dunia na Ubingwa wa Ulaya mara mbili. Lakini safari yake ya soka ilianza Sevilla kabla ya kununuliwa na Real Madrid, na hatimaye alirejea tena katika klabu yake ya kwanza.

Na sasa ripoti zinaonyesha yuko tayari kuinunua klabu ya Sevilla.

Gazeti la Estadio Deportivo linaripoti kuwa Ramos, ambaye tayari ni mshauri wa klabu na ana idadi ndogo ya hisa, anafikiria kuwa mwekezaji katika mauzo yajayo ya klabu hiyo.

Wanasema kuwa kwa sasa, beki huyo nguli “amekuwa akiomba taarifa tu kuhusu chaguo zake endapo ataamua kununua sehemu kubwa ya hisa.”

Uwanjani, Sevilla imekuwa ikipitia kipindi kigumu katika mashindano ya ndani hivi karibuni. Kwa sasa inashika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa LaLiga, na katika misimu ya hivi karibuni wamekuwa wakijikuta zaidi nusu ya chini ya msimamo.

Mabingwa wa mara nyingi wa Europa League, waliotwaa kombe hilo mara ya mwisho msimu wa 2022/23 na sasa wanatumaini kurejea katika mafanikio yao ya zamani. Walimaliza mwaka 2025 kwa kipigo kutoka kwa Real Madrid na wanatarajia 2026 uwe mwaka mkubwa, ndani na nje ya uwanja. Mechi za nyumbani dhidi ya Levante na Celta Vigo mfululizo zitafungua kalenda mpya ya mwaka huu wa 2026.