Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Schumacher majeruhi lakini hayupo kitandani

SHUMA Pict

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa taarifa mpya zilizofichuliwa na Daily Mail, Schumacher (57), raia wa Ujerumani na bingwa mara saba wa dunia wa F1 anaendelea kuishi maisha ya faragha tangu alipoumia kichwa baada ya kugonga mwamba katika eneo la mapumziko la Meribel, Ufaransa.

MALLORCA, HISPANIA: GWIJI wa mashindano ya Formula One (F1), Michael Schumacher ambaye alipata ajali mbaya katika mchezo wa kuteleza kwenye theluji miaka 12 iliyopita anaripotiwa kuwa siyo mgonjwa wa kulazwa kitandani tena.

Kwa mujibu wa taarifa mpya zilizofichuliwa na Daily Mail, Schumacher (57), raia wa Ujerumani na bingwa mara saba wa dunia wa F1 anaendelea kuishi maisha ya faragha tangu alipoumia kichwa baada ya kugonga mwamba katika eneo la mapumziko la Meribel, Ufaransa.

Hali yake ya kiafya imekuwa siri inayojulikana kwa wanafamilia wa karibu na marafiki wachache walioteuliwa kwa uangalifu.

Vyanzo vya karibu na familia hiyo vinaeleza kuwa Schumacher kwa sasa anakaa kwenye kiti cha magurudumu, na anaweza kusukumwa kuzunguka ndani ya jumba lake la kifahari lenye thamani ya Pauni 30 milioni 30 huko Mallorca pamoja na makazi yake mengine ya Pauni 50 milioni yaliyopo Gland, kando ya Ziwa Geneva nchini Uswisi.

SHU 01

Kwa mujibu wa taarifa hizo, dereva huyo  anahudumiwa kwa karibu na mkewe Corinna, ambaye wamekuwa kwenye ndoa kwa miaka 30, akisaidiwa na timu ya wauguzi na wataalamu wa tiba wanaofanya kazi kwa zamu saa 24 kwa siku. Gharama za huduma hiyo inadaiwa kufikia makumi ya maelfu ya pauni kwa wiki.

Faragha ya Schumacher inaelezwa kuwa kipaumbele kikubwa kwa familia. Tangu ajeruhiwe ubongo hajawahi kuonekana hadharani. Mwaka jana, wafanyakazi wa zamani walihukumiwa baada ya kujaribu kuuza picha za Schumacher akiwa dhaifu kiafya.

Wakati huohuo, familia imekuwa ikikanusha taarifa potofu ikiwemo madai kuwa alihudhuria harusi ya binti yake, Gina 2024 ikida kuwa hazina ukweli wowote.

Uvumi uliodai kuwa Schumacher alikuwa anaugua pseudocoma (ugonjwa unaotokana na majeraha ya ubongo, mshtuko mkubwa au matatizo ya mfumo wa neva, ambapo mgonjwa huwa na fahamu lakini hawezi kuwasiliana isipokuwa kwa kupepesa macho), siyo wa kweli.

SHU 02

Vyanzo kadhaa vya karibu vimethibitisha kuwa madai hayo hayana uhalisia

“Hisia iliyopo ni kwamba anaelewa baadhi ya mambo yanayoendelea karibu yake, lakini huenda siyo yote,” kilisema chanzo kimoja cha karibu na familia hiyo.

Licha ya maendeleo hayo madogo, hali ya Schumacher inaendelea kuwa siri kubwa, huku familia ikisisitiza heshima, subira na faragha kwa ajili ya mmoja wa wanamichezo bora zaidi katika historia ya michezo ya mbio za magari duniani.