Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Scholes amtaja mchezaji mbovu Man United

SCHOLES Pict

Muktasari:

  •  Scholes alicheza kwa takribani miaka 20 katika kikosi cha Man United, ambapo alikuwa sehemu  muhimu ya safu ya kiungo ya timu hiyo chini ya Sir Alex Ferguson.

MANCHESTER, ENGLAND: NGULI wa Manchester United, Paul Scholes, ametaja usajili mbaya zaidi kuwahi kufanywa na klabu hiyo, huku akimkosoa aliyekuwa mchezaji mwenzake kwa kukosa uelewa wa mpira wa miguu.

 Scholes alicheza kwa takribani miaka 20 katika kikosi cha Man United, ambapo alikuwa sehemu  muhimu ya safu ya kiungo ya timu hiyo chini ya Sir Alex Ferguson.

Alifanikiwa kushinda mataji 11 ya Ligi Kuu England, FA Cup matatu, pamoja na Ligi ya Mabingwa Ulaya mara mbili.

Kupitia kipindi cha  The Overlap, Scholes amemtaja  golikipa Mark Bosnich kama moja kati ya usajili mbaya zaidi wa Manchester United kuwahi kufanyika wakati yeye akiwa katika timu hiyo na akamkosoa kwa kushindwa hata kupiga mpira kiusahihi.

“Wakati nilipokuwa najaribu kutazama nani atamrithi Peter Schmeichel, mimi mwenyewe nilikuwa napata kigugumizi. Katika timu tulikuwa na makipa wachache, binafsi nilikuwa nikiwafikiria Massimo Taibi na Mark Bosnich. Nilidhani Mark alikuwa golikipa mzuri kwa kile alichoonyesha akiwa Aston Villa. Mambo yalibadilika sana alipokuja kwetu, alionyesha kiwango cha hovyo, ilinishangaza sana. Kulikuwa na mazoezi ya kupiga mashuti, kwa kawaida mchezaji ilitakiwa upige mashuti 15 au 20. Baada ya mashuti matatu tu, tayari alikuwa amechoka, alikuwa akisema ‘Hapana, aje mtu mwingine.”

SCH 01
SCH 01

“Sijawahi kuona kitu kama hicho. Kuna siku tulicheza na Everton ugenini kwenye mechi ya kwanza ya msimu, Mark hakuweza kufikisha mpira hata kwenye mstari wa kati kati ya uwanja. Hakukuwa na upepo, ilikuwa siku nzuri kabisa. Lakini ukiangalia miguu yake, alikuwa na viatu namba 14; kwa kweli alikuwa anapiga ardhi muda wote, miguu mikubwa kama makasia. Kwa kweli ilisikitisha sana.”

Bosnich awali alisajiliwa na Man United mwaka 1990, kabla ya kurejea Australia na baadaye kurudi tena Ligi Kuu ya England mwaka 1992 alipojiunga na Aston Villa.

Golikipa huyo wa kimataifa wa Australia alikaa miaka saba Aston Villa kama chaguo la kwanza langoni, na kiwango chake kizuri kikamfanya arejee tena Man United mwaka 1999.

Bosnich alikuwa kipa namba moja wa Manchester United katika msimu wa ubingwa wa 1999/2000, lakini alipoteza nafasi yake mbele ya  Fabien Barthez msimu uliofuata.