Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Samir Nasri akamatwa, kuhojiwa kwa saa 10

SAMIR Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo wa zamani wa Ligi Kuu England amejikuta akihusishwa na uchunguzi mpana unaofanywa na polisi kuhusu madai ya uhusiano na mtandao wa kihalifu unaodaiwa kuongozwa na mfanyabiashara wa dawa za kulevya kutoka Marseille ambaye kwa sasa anatumikia kifungo gerezani.

PARIS, UFARANSA: NYOTA wa zamani wa Arsenal na Manchester City, Samir Nasri, ameripotiwa kukamatwa na kuhojiwa na polisi wa Ufaransa katika uchunguzi wa tuhuma za utakatishaji fedha zinazodaiwa kuhusishwa na kinara wa mtandao wa biashara ya dawa za kulevya anayejulikana kwa jina la "Wild Boar".

Nyota huyo wa zamani wa Ligi Kuu England amejikuta akihusishwa na uchunguzi mpana unaofanywa na polisi kuhusu madai ya uhusiano na mtandao wa kihalifu unaodaiwa kuongozwa na mfanyabiashara wa dawa za kulevya kutoka Marseille ambaye kwa sasa anatumikia kifungo gerezani.

Kwa mujibu wa Le Parisien, Nasri, ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka katika kituo cha televisheni cha Canal Plus, alihojiwa kwa takribani saa 10 na maafisa wa polisi Alhamisi.

SAMI 01

Mahojiano hayo yalikuwa sehemu ya uchunguzi mkubwa unaohusu tuhuma za uingizaji wa dawa za kulevya, kuunda genge la uhalifu pamoja na utakatishaji wa fedha zinazodaiwa kupatikana kupitia biashara ya dawa za kulevya.

Hata hivyo, Nasri mwenye umri wa miaka 39 aliachiwa huru jioni ya Alhamisi bila kufunguliwa mashtaka yoyote, huku mpaka sasa hakuna hatua za kisheria zilizochukuliwa dhidi yake.

Wachunguzi wanachunguza madai ya uhusiano kati ya Nasri na mtandao wa kihalifu unaomhusu Hakim Berrebouh, anayefahamika kwa jina la utani la "Wild Boar", ambaye amekuwa gerezani tangu mwaka 2021 kwa makosa yanayohusiana na biashara ya dawa za kulevya.

Katika uchunguzi huo pia ametajwa Olivier Sabbah maarufu kama "Paulo", ambaye anadaiwa kuwa mmoja wa watu muhimu katika mtandao wa utakatishaji fedha unaohusishwa na shughuli za kihalifu za Berrebouh.

SAMI 02

Kwa mujibu wa taarifa hizo, polisi wanachunguza iwapo Nasri alihusika katika upande wa utakatishaji fedha kupitia klabu ya usiku ya XS, iliyopo Ivry-sur-Seine, mkoani Val-de-Marne.

Nasri alikuwa mmoja wa wanahisa wa klabu hiyo mwaka 2016 baada ya kuwekeza mamia ya maelfu ya euro, kipindi ambacho alikuwa akilipwa mamilioni ya euro akiwa mchezaji wa Manchester City.

Baadaye, kiungo huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa alikuja kuwa mmiliki mwenza wa klabu hiyo pamoja na Bilele Z., ambaye anadaiwa kuwa mmoja wa washirika wake wa karibu na pia alikamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi Alhamisi.

Mpaka sasa, Nasri hajafunguliwa mashtaka yoyote, huku uchunguzi wa polisi ukiendelea kubaini kama kuna ushahidi wa kuhusika kwake katika tuhuma hizo.