Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Saliba afunguka kuikacha Real Madrid

SALIBa Pict

Muktasari:

  • Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 24, amesaini mkataba mpya wa miaka mitano kuendelea kusalia Emirates ambao utakuwa na ongezeko pia la mshahara.

LONDON, ENGLAND: BEKI kisiki wa Arsenal, William Saliba ameweka wazi kwamba alikataa kujiunga na Real Madrid na kuendelea kubalia Arsenal kwa sababu bado hajakamilisha jambo moja ambalo ni kushinda mataji na washika mitutu hao.

Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 24, amesaini mkataba mpya wa miaka mitano kuendelea kusalia Emirates ambao utakuwa na ongezeko pia la mshahara.

Saliba ameulizwa kwanini hakuchukua uamuzi wa kuondoka kama alivyofanya beki wa Liverpool Trent Alexander-Arnold alipoamua kuondoka Liverpool katika dirisha lililopita kujiunga na Real Madrid.

"Lakini yeye alishinda mataji akiwa na Liverpool. Mimi? Sijashinda chochote hapa isipokuwa… ni kikombe gani tulishinda? lLabda Ngao ya Jamii. Kwa hiyo, ndiyo, ni Ngao ya Jamii pekee. Sijafanya jambo lolote kubwa kwa klabu hii hadi sasa. Siwezi kuondoka hapa bila kuipa klabu kitu cha maana. Chaguo langu la kwanza lilikuwa kusalia na kushinda kila kitu kwanza."

SALI 01

Saliba ameendelea kusisitiza: "Tumekuwa karibu kushinda mataji mara nyingi lakini tunafeli na naamini huwa kuna upungufu lakini kila mwaka tunazidi kuwa bora. Tumepata uzoefu wa kutosha kutoka katika misimu mitatu iliyopita. Kwa hiyo sasa ni wakati wa kuacha maneno na kuthibitisha uwanjani kwamba tunaweza kushinda mataji makubwa. Kila mwisho wa msimu unapomaliza nafasi ya pili, unajisikia hasira kidogo. Huwa nataka kwenda likizo na kusherehekea na marafiki kwa mataji niliyoshinda."

Mkataba mpya wa Saliba unamfanya alipwe mshahara wa takribani Pauni 250,000 kwa wiki.

SALI 02

Mbali ya Saliba, Arsenal tayari imewasainisha mkataba mpya Martin Odegaard na Ben White ambayo itamalizika mwaka 2028.

Dirisha lililopita la majira ya kiangazi, Gabriel Magalhaes, 27, alisaini mkataba mpya utakaomalizika mwaka 2029, huku chipukizi Myles Lewis-Skelly na Ethan Nwaneri wakisaini hadi mwaka 2030.