Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Saliba aifungia vioo Real Madrid

SALIBa Pict

Muktasari:

  • Saliba ambaye ni miongoni mwa wachezaji tegemeo wa Arsenal amekuwa akiwindwa na Madrid tangu mwaka jana na ilielezwa kuwa iliwasilisha hadi ofa kwa ajili ya kumsajili lakini ilikataliwa.

LONDON, ENGLAND: BEKI kisiki wa Arsenal, William Saliba ameifungia vioo Real Madrid na kuamua kufikia makubaliano ya kusaini mkataba mpya na washika mitutu.

Saliba ambaye ni miongoni mwa wachezaji tegemeo wa Arsenal amekuwa akiwindwa na Madrid tangu mwaka jana na ilielezwa kuwa iliwasilisha hadi ofa kwa ajili ya kumsajili lakini ilikataliwa.

Licha ya ofa hiyo kukataliwa, Madrid bado iliendelea kupambana kwa ajili ya kumsajili Saliba na ilikuwa na matumaini kwa sababu mkataba wake ulikuwa unaisha 2027.

Arsenal ilianza mazungumzo ya mkataba mpya na beki huyu tangu Mei mwaka huu na kocha Mikel Arteta alikuwa akiwasisitiza kwamba wapambane kuhakikisha wanambakisha kwani ni mchezaji muhimu.

Real Madrid ilikuwa ikimshawishi asikubali kusaini mkataba huo mpya ili impate kwa bei chee ifikapo mwakani jambo ambalo imekuwa ikilifanya kwa wachezaji wengi hivi karibuni.

Hata hivyo, Saliba alikataa kwani anaona anajisikia furaha zaidi kuendelea kusalia katika kikosi cha Arsenal, hivyo amemua kusaini mkataba mpya.

Msimu uliopita Saliba, alicheza mechi 51 akiisaidia Arsenal kumaliza katika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu England kwa mara ya tatu mfululizo pamoja na kufika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Saliba alisajiliwa na Arsenal mwaka 2019. akitokea Saint-Etienne wakati huo kocha akiwa ni Mhispania, Unai Emery na hadi sasa hajawahi kushinda taji lolote na washika mitutu hao.

Hata hivyo, uwepo wake katika safu ya ulinzi ya Arsenal, imeifanya  timu hiyo kujijengea sifa ya kuwa na moja ya safu bora za ulinzi barani Ulaya kwa sasa,

Akihojiwa Julai mwaka huu kuhusu uwezekano wa kusaini mkataba mpya, Saliba alisema: ”Ndiyo, natumai kusaini ingawa bado hakuna makubaliano rasmi yaliyofikiwa, lakini kuna mazungumzo mazuri kati yangu, wakala wangu na klabu.” Tutaona hapo baadae.”