Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Salah mwaka mmoja freshi tu

Muktasari:

  • Winga huyo wa kimataifa wa Misri mkataba wake wa sasa huko Merseyside utafika tamati mwishoni mwa msimu huu na aliweka wazi Liverpool bado hajaweka mezani ofa yoyote mpya ya mkataba mpya kutokana na kuweka ugumu kwenye kutibua mfumo wao wa bili za mishahara.

LIVERPOOL, ENGLAND: SUPASTAA, Mohamed Salah amefungua milango ya kuongeza mwaka mmoja kwenye mkataba wake huko Liverpool – licha ya klabu hiyo kumvuruga kwa kushindwa kumalizana haraka juu ya jambo hilo.

Winga huyo wa kimataifa wa Misri mkataba wake wa sasa huko Merseyside utafika tamati mwishoni mwa msimu huu na aliweka wazi Liverpool bado hajaweka mezani ofa yoyote mpya ya mkataba mpya kutokana na kuweka ugumu kwenye kutibua mfumo wao wa bili za mishahara.

Julai 2022, Salah alisaini mkataba wa miaka mitatu unaomshuhudia akilipwa Pauni 350,000 kwa wiki – na staa huyo anaamini mshahara wake utapanda wakati atakaposaini dili jipya la kuendelea kubaki kwenye kikosi hicho.

Kwa mujibu wa The Athletic, Salah, 32, yupo tayari kusaini mkataba wa mwaka mmoja ili kumaliza utata wa sasa wa kuhusu dili jipya ili atulize akili yake kwenye mapambano ya kuipa Liverpool taji la Ligi Kuu England msimu huu.

Kipaumbele chake kwa sasa ni kubaki kwenye klabu ambayo aishinda taji la Ligi Kuu England, Ligi ya Mabingwa Ulaya, Uefa Super Cup, Fifa Club World Cup, Kombe la FA, Kombe la Ligi na kufunga mabao 224 kwenye mechi 369.

Mazungumzo ya dili jipya bado hayajafanyika, Liverpool ikiwa inajitathmini kwanza kitu ambacho kinadaiwa kumvuruga Mo Salah.

Kutokana na hilo, Mo Salah alithubutu kusema anajiona kama anaondoka kuliko kubaki kwenye timu, kauli aliyoitoa kwenye mechi ya ushindi wa mabao 3-2 kwenye Ligi Kuu England dhidi ya Southampton, Novemba 24.

Baada ya mechi ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Manchester City wikiendi iliyopita – aliyofunga na kuasisti – alidai hiyo inaweza kuwa mechi yake ya mwisho kukabiliana na chama hilo la Pep Guardiola uwanjani Anfield.

Salah atakuwa huru kuzungumza na klabu za nje kuanzia Januari Mosi kwa ajili ya kusaini dili la awali huku vigogo Paris Saint-Germain, ikiwa ni miongoni mwa timu zinazotaka huduma yake ikiwamo timu za Saudi Arabia, ikiwamo Al-Ittihad, ambayo iliweka mezani Pauni 150 milioni kwenye dirisha la kiangazi mwaka 2023.