Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ishu ya ubingwa EPL, kompyuta imeganda kwa Arsenal

KOMPUTA Pict

Muktasari:

  • Huu unaonekana unaweza kuwa mwaka wa Kocha Mikel Arteta na chama lake la Arsenal kumaliza msimu kwenye kilele cha msimamo wa Ligi Kuu England baada ya kutoka kapa kwa misimu mitatu mfululizo.

LONDON, ENGLAND: KOMPYUTA janja bado imeitabiria Arsenal kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu mbele ya Manchester City.

Huu unaonekana unaweza kuwa mwaka wa Kocha Mikel Arteta na chama lake la Arsenal kumaliza msimu kwenye kilele cha msimamo wa Ligi Kuu England baada ya kutoka kapa kwa misimu mitatu mfululizo.

Licha ya kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Sunderland katika mchezo uliopita, kompyuta maalumu ya AceOdds.com, bado imeitabiria timu hiyo itamaliza nafasi ya kwanza kwenye Ligi Kuu England msimu huu pointi saba juu ya Man City itakayomaliza namba mbili.

Man City ya kocha Pep Guardiola iliichapa Liverpool 3-0 katika mchezo huo wa ligi uliofanyika Jumapili na kufanya pengo la pointi kubakia nne tu katika kuwafikia Arsenal.

Kom 02

Kipigo hicho kwa Liverpool kilikuwa cha tano kwenye mechi 11 ilizocheza Ligi Kuu England msimu huu, lakini kompyuta hiyo ya kijanja haijaifuta timu hiyo ya Arne Slot kwenye mbio za ubingwa, lakini itamaliza nafasi ya tatu, pointi nane nyuma ya bingwa.

Timu inayoshika nafasi ya tatu kwa sasa kwenye msimamo wa ligi, Chelsea yenyewe itashuka kwa nafasi moja hadi namba nne kwa mujibu wa utabiri huo wa kumpyuta licha ya ushindi wao mnono dhidi ya Wolves iliyopata Jumamosi iliyopita.

Chama la Ruben Amorim, Manchester United limetabiriwa litaendelea kupambana na msimu huu kompyuta imedai itamaliza ligi kwenye nafasi ya tano, tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita na miamba hiyo ya Old Trafford ilimaliza nafasi ya 15 na kushindwa kushiriki kwenye michuano yote ya Ulaya.

Kom 01

Kompyuta imedai Crystal Palace itamaliza msimu kwenye nafasi ya sita na hivyo kukamatia tiketi ya kucheza michuano ya Europa League, wakati Tottenham itaungana na Bournemouth na Newcastle kwenye nafasi ya nane, tisa na 10, huku zikilingana pointi na kwamba zitatofautiana kwa mabao tu. Spurs iligomewa kupata ushindi mbele ya Man United, Jumamosi iliyopita baada ya beki Matthijs De Ligt kufunga bao la kusawazisha dakika za majeruhi, huku Newcastle iliendelea na rekodi yao mbovu baada ya kuchapwa 3-1 na Brentford.

Mashabiki wa Sunderland watakuwa wenye huzuni baada ya kikosi chao kutabiriwa kwamba kitamaliza msimu kwenye nafasi ya 15 licha ya kuwa na mwanzo mzuri wa msimu. Timu hiyo iliyopanda daraja msimu huu, ilitibua rekodi ya Arsenal ya kucheza mechi nyingi bila ya kuruhusu bao kwenye nyavu zao.