Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sababu ya Ronaldo kukataa Kombe la Dunia la Klabu

RONALDO Pict

Muktasari:

  • Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 40 alikuwa akihusishwa sana na kuondoka Al Nassr na alishapokea ofa kadhaa lakini alikataa na kuamua kusalia.

RIYADH, SAUDI ARABIA: NYOTA wa Al Nassr ambaye amesaini mkataba mpya wa miaka miwili wa kuendelea kuitumikia timu hiyo, Cristiano Ronaldo amefichua sababu za kukataa ofa ya kwenda kucheza michuano ya Kombe la Dunia la klabu linaloendelea huko Marekani.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 40 alikuwa akihusishwa sana na kuondoka Al Nassr na alishapokea ofa kadhaa lakini alikataa na kuamua kusalia.

Inaelezwa Ronaldo anatarajiwa kuvuna kiasi cha pauni  492 milioni kama mshahara katika kipindi cha miaka hiyo miwili ya mkataba huo unaotarajiwa kuwa ghali zaidi katika soka.

Ronaldo amesema kuwa alikataa ofa hiyo kwa sababu ana nia ya kushinda mataji zaidi akiwa na Al-Nassr, huku taji lake pekee alilonalo hadi sasa alilochukua ndani ya timu hiyo ni Kombe la Mabingwa wa Klabu za Kiarabu waliloshinda mwaka 2023.

“Nilikuwa na ofa za kucheza Kombe la Dunia lakini nadhani haikuwa na maana kwa sababu napendelea kuwa na mapumziko mazuri, maandalizi mazuri kwa sababu msimu ujao utakuwa mrefu sana kwani kuna Kombe la Dunia hapo mwakani. Nataka kuwa tayari si kwa ajili ya Al-Nassr tu bali pia kwa timu ya taifa, ndiyo maana niliamua kucheza mechi ya mwisho ya Nations League na kukataa ofa niliyopewa.”

Aidha, Ronaldo alisema anaamini kuwa Ligi Kuu ya Saudi Arabia ni miongoni mwa ligi tano bora duniani na kila siku zinavyozidi kwenda inazidi kukua.

“Bado tunaboresha lakini naamini tayari tuko kwenye tano bora. Bado naamini tunaendelea kuboresha na tuna muda wa kufanya hivyo. Tumekuwa tukionyesha kwa miaka miwili iliyopita kwamba ligi inapanda kila wakati, kwa hiyo nina furaha. Ni wale tu ambao hawaelewi chochote kuhusu mpira ndio husema ligi hii haimo kwenye tano bora. Ninaamini kwa asilimia 100 katika maneno yangu hii ni ligi bora ndio maana nataka kubaki.”

Inaelezwa Ronaldo alipata ofa ya kujiunga na Al-Hilal iende naye katika Kombe la Dunia la Klabu.