Sababu ya Garnacho kutoitwa Argentina

LONDON, ENGLAND. KOCHA wa tmu ya taifa ya Argentina, Lionel Scaloni amefichua kwanini hakumjumuisha kinda wa Manchester United, Alejandro Garnacho kwa ajili ya mechi za kimataifa.

Wakati orodha ya wachezaji wa timu ya taifa ilipotajwa wiki iliyopita, winga huyo wa United hakujumuishwa, lakini winga wa Benfica, Angel di Maria ameitwa badala yake, huku Paulo Dybala ambaye alipona majeraha amerejea kikosini.

Kocha huyo amedokeza kwamba sababu ya kutomjumuisha Garnacho kikosini ni kutokana na kiwango kibovu alichoonyesha kwenye mechi za hivi karibuni, lakini maswali mengi yameibuka kutokana na uamuzi wa kocha huyo wa Argentina.

Scaloni aliwaambia waandishi wa habari: “Kutoitwa Garnacho kunatokana na kiwango chake. hakuwa na muda mwingi wa kucheza hivyo lazima tufikirie maslahi ya timu kwanza. Yuko kwenye rada yetu na atakuwa sehemu ya mipango yetu kwani bado tunamfuatilia mwenendo wake.”

Kocha wa Man United, Erik ten Hag huenda atakuwa amefarijika kwamba Garnacho hajajumuishwa kwenye kikosi cha Argentina kutokana na majeraha yanayoendelea kuwaandama msimu huu.

Licha ya kutokuwa fiti, Garnacho ni mmoja wa washambuliaji hodari wa United mwenye kipaji.

Garnacho ana uwezo wa kucheza na Marcus Rashford na Rasmus Hojlund kwenye safu ya ushambuliaji ambayo msimu huu imeonekana kuwa butu.

Katika kipindi hiki cha mapumziko, Garnacho atakuwa na muda wa kuendelea na mazoezi chini ya kocha wao Ten Hag.