Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ruben Amorim: Sikuwa na hofu ya kufukuzwa kazi

AMORIM Pict

Muktasari:

  • Ratcliffe alitoka hadharani kumpa sapoti kocha huyo mkuu wa Man United na kusema hawezi kumfukuza na anaamini ataifikisha timu hiyo katika nchi ya ahadi.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester United, Ruben Amorim amesisitiza hajawahi kuwa na hofu juu ya kufukuzwa kazi na tajiri na mmiliki wa timu hiyo, Sir Jim Ratcliffe na presha za kuondolewa kwake zilitoka kwa mashabiki na watu wa nje.

Maswali kuhusu hatima ya Amorim yaliongezeka zaidi baada ya kipigo dhidi ya Brentford na Manchester City ugenini.

Ratcliffe alitoka hadharani kumpa sapoti kocha huyo mkuu wa Man United na kusema hawezi kumfukuza na anaamini ataifikisha timu hiyo katika nchi ya ahadi.

Mashabiki wengi walionekana kukata tamaa na Amorim na baadhi wakikosoa sana mfumo na mbinu zake wakimtaka azibadilishe lakini mwenyewe aliendelea kusisitiza hatobadili falsafa zake hata iweje.

AMO 01

Baada ya msururu wa matokeo mabovu, hatimaye hivi karibuni mambo yalionekana kujipa kwa mashetani hao wekundu ambao sasa wameshinda mechi tatu mfululizo za Ligi Kuu England.

"Sijawahi kuwa na mawazo ya kufukuzwa kwa sababu ya kutoshinda mechi, shinikizo kubwa la mimi kufukuzwa kazi lilikuwa linatengenezwa na mashabiki, lakini hali ilikuwa tofauti kwa Jim, muda wote yeye anaamini na anajua tunachokifanya lakini kwa mashabiki wao ilikuwa tofauti, wanahitaji matokeo tu," amesema Amorim.

AMO 02

Wikiendi iliyopita, Man United ilipata ushindi wa mabao 4-2 kutoka kwa Brighton na Bryan Mbeumo ndio alionekana kuwa na hatari zaidi akifunga mabao mawili, wakati Casemiro na Matheus Cunha wakifunga bao moja kila mmoja.

Alipoulizwa kama sasa wachezaji wake wameanza kuelewa mfumo wake na kama hiyo ndiyo siri ya mabadiliko ya kiwango cha timu yake, Amorim amesema: "Kuelewa mfumo wangu ilikuwa muhimu sana kabla ya vyote. Nafikiri wachezaji wanaelewa vizuri mfumo wangu na kila kitu wanachotakiwa kufanya."

AMO 03

Mechi ijayo, Man United itasafiri kwenda Nottingham kwa ajili ya kuvaana na Nottingham Forest katika Ligi Kuu England.

Amorim aliongeza siri ya mafanikio ya timu ni wachezaji kuwa na imani na anaamini tangu kuanza kwa msimu huu walikuwa na kikosi bora na kucheza vizuri, tofauti ni wachezaji hawakuwa wamezoea baadhi ya vitu.