Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ruben Amorim:  Kobbie Mainoo anatakiwa kupambana

AMORIM Pict

Muktasari:

  • Hatima ya Mainoo ndani ya Old Trafford bado haijulikani baada ya nyota huyo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 20 kukataliwa ombi lake la kuondoka katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester United, Ruben Amorim amemtaka kiungo wa timu hiyo Kobbie Mainoo kupigania nafasi yake ndani ya Manchester United kama walivyofanya magwiji wa timu hiyo, Cristiano Ronaldo na Wayne Rooney.

Hatima ya Mainoo ndani ya Old Trafford bado haijulikani baada ya nyota huyo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 20 kukataliwa ombi lake la kuondoka katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Staa huyu anahusishwa kuondoka Januari ambapo Napoli ni kati ya timu 12 zinazohitaji saini yake.

"Kobbie anatakiwa kupigania nafasi yake. Sio jambo baya kukaa benchini katika timu kama Manchester United ukiwa na umri wa miaka 20. Ninakumbuka Ronaldo aliwahi kuwa benchi, Rooney pia alikuwa benchi wakati mwingine. Juan Sebastian Veron hakuwa akicheza. Nakumbuka historia yote ya Man United.

AMO 01

"Sisemi kwamba yeye ni mchezaji mkubwa hivyo anatakiwa kukaa benchi kama walivyowahi kukaa hao wengine. Hapana, hapana. Ninachosema ni kinyume chake. Nataka tu kusaidia timu ishinde na kumsaidia Kobbie awe mchezaji bora zaidi."

Katika umri wa Mainoo, Ronaldo alikuwa anaanza takribani asilimia 80 ya mechi za Man United, akikaa benchi mara chache pale Sir Alex Ferguson alipokuwa akicheza kwa mtindo wa kujilinda.

Maswali kuhusu Veron yaliwahi kumfanya Fergie kushambulia vikali vyombo vya habari, maneno ambayo ni ngumu kuandikwa.

Amorim amesema kuwa moja kati ya mambo yanayosababisha Mainoo asipate sana nafasi ni kwa sababu anacheza namba moja na Bruno Fernandes, ingawa hilo linaonekana kupingwa na wadau wengi kwani staa huyo alicheza sambamba na Bruno katika mechi ya Jumatatu wiki iliyopita dhidi ya Bournemouth katika dakika 30 za mwisho mechi ambayo ilimalizika kwa sare ya mabao 4-4.

AMO 02

Man United ina machaguo machache katika safu yao ya ushambuliaji baada ya Bryan Mbeumo na Amad Diallo kuondoka kwenda kwenye majukumu ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

Hali hiyo inaongeza matumaini ya Mainoo kupata nafasi yake ya kwanza ya kuanza katika Ligi Kuu England tangu Mei mwaka huu.

Amorim alikataa kuzungumzia moja kwa moja suala la kaka wa Mainoo, Jordan kuvaa fulana yenye ujumbe wa “Free Kobbie” Jumatatu usiku.

Kocha huyo raia wa Ureno amesema: "Niliwahi kuwa na hali kama hiyo nilipokuwa Sporting na kaka yangu aliandika kitu mtandaoni na nililazimika kujibu kwa niaba yake. Maelezo yangu yalikuwa kwamba ana maisha yake, ana maoni yake, na hayo yote hayahusiani na mimi. Kwa hiyo nasema hivyo hivyo kwa Kobbie."