Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Manchester United yamnasa Andrey Santos

SANTOS Pict

Muktasari:

  • Santos mwenye umri wa miaka 22 tayari amekubaliana masharti binafsi na United, huku Chelsea ikimpa ruhusa ya kusafiri kwenda Manchester kwa ajili ya vipimo vya afya kabla ya kukamilisha uhamisho huo.

LONDON, ENGLAND: MANCHESTER United imefikia makubaliano na Chelsea ya kumsajili kiungo wa kimataifa wa Brazil, Andrey Santos, kwa ada ya pauni50 milioni.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, United italipa pauni 48milioni kama ada ya msingi, huku pauni milioni mbili zikiongezwa kama bonasi zinazotarajiwa kufikiwa kirahisi. Chelsea nayo imehakikisha inaweka kipengele cha asilimia 10 ya mauzo ya baadaye ya mchezaji huyo.

Santos mwenye umri wa miaka 22 tayari amekubaliana masharti binafsi na United, huku Chelsea ikimpa ruhusa ya kusafiri kwenda Manchester kwa ajili ya vipimo vya afya kabla ya kukamilisha uhamisho huo.

SANTO 01

Licha ya kuwa na mkataba Stamford Bridge hadi mwaka 2030 na kuvutia klabu kadhaa, Santos ameona nafasi ya kucheza mara kwa mara ni finyu Chelsea, hasa baada ya Moises Caicedo kuongeza mkataba wake hadi mwaka 2033 mwezi Aprili.

Kiungo huyo alijiunga na Chelsea akitokea Vasco da Gama ya Brazil Januari 2023, na katika msimu wa 2025/26 alicheza mechi 43 katika mashindano yote, akifunga mabao matatu na kutoa asisti nne.

Santos tayari ameichezea timu ya taifa ya Brazil mara sita, lakini hakujumuishwa kwenye kikosi cha kocha Carlo Ancelotti kilichoshiriki Kombe la Dunia la mwaka huu.

SANTO 02

Baada ya kuwasili Chelsea, alianza kwa kutolewa kwa mkopo Nottingham Forest katika nusu ya kwanza ya msimu wa 2023/24, ambako alipata nafasi ya kucheza mechi mbili pekee. Baadaye alitumia miezi 18 kwa mkopo Strasbourg ya Ufaransa, ambako aling'ara kwa kufunga mabao 12 na kutoa asisti tano katika mechi 45.

United, ambayo itashiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu, imeweka kipaumbele cha kuimarisha safu ya kiungo baada ya kubaini eneo hilo linahitaji maboresho makubwa.

Mbali na Santos, tayari klabu hiyo imefikia makubaliano ya kumsajili kiungo Ederson kutoka Atalanta kwa pauni35 milioni, ingawa kukamilika kwa dili hilo kumechelewa kutokana na mchezaji huyo kuitwa ghafla kwenye kikosi cha Brazil kilichoshiriki Kombe la Dunia.

SANTO 03

Vyanzo vya ndani ya Manchester United vimekanusha taarifa zilizoibuka mwishoni mwa wiki zikidai kuwa dili la Ederson limevunjika, vikisisitiza kuwa usajili huo bado upo mezani na vipimo vya afya vinatarajiwa kufanyika katika wiki zijazo baada ya Brazil kutolewa na Norway kwa mabao 2-1 katika hatua ya 16 Bora ya Kombe la Dunia.

United imeamua kuongeza nguvu eneo la kiungo baada ya Casemiro kuondoka klabuni na Manuel Ugarte kupata majeraha ya kano za goti wakati Uruguay ilipocheza dhidi ya Hispania katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Kombe la Dunia.

Mbali na Santos na Ederson, majina mengine yaliyowahi kuingia kwenye rada za United ni Aurelien Tchouameni wa Real Madrid, Carlos Baleba wa Brighton na Adam Wharton wa Crystal Palace.