Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Magwiji waungana ishu ya Mainoo

Muktasari:

  • Kiungo Mainoo amekuwa na wakati mgumu kikosini Man United, ambako amekuwa akisugua benchi chini ya kocha Amorim.

MANCHESTER, ENGLAND: RIO Ferdinand ameungana na Paul Scholes kumkosoa kocha Ruben Amorim kutokana na kile anachomfanyia Kobbie Mainoo na hivyo kumtaka zao hilo la akademia ya Manchester United kuondoka kwenye klabu hiyo.

Kiungo Mainoo amekuwa na wakati mgumu kikosini Man United, ambako amekuwa akisugua benchi chini ya kocha Amorim.

Kocha huyo wa Man United, Amorim amekuwa akiwatumia Casemiro na Bruno Fernandes kwenye eneo hilo la kiungo, hivyo kumfanya Mainoo kucheza mechi 10 tu kwenye Ligi Kuu England ambazo amekuwa akitokea benchini.

Mainoo, 20, alikaribia kuondoka kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi na yupo tayari kwenda kujiunga kwa mkopo huko Napoli kwenye dirisha lijalo la Januari ili kupata nafasi ya kucheza akitafuta namna ya kupata namba katika kikosi cha England kitakachokwenda kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026.

Mainoo alicheza kwa dakika 12 tu akitokea benchini kwenye ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Wolves, Jumatatu iliyopita.

Kutokana na Amorim kumweka benchini muda mwingi kiungo huyo imewaamsha magwiji wa Man United na kuingilia kati.

Rio alisema: “Niliwaona (Nicky) Butty na (Paul) Scholes wakizungumzia juu ya hili na nakubaliana nao. Kama nitafikiria hilo na nikijiweka kwenye viatu vya Kobbie Mainoo, najiona nipo nje, nitaondoka.

“Alikuwa akiichezea England na alikuwa mmoja wa wachezaji bora kwenye mashindano. Sio watu wengi wanaweza kusemea hilo. Amepoteza tu miezi 18 ya maisha yake ya soka hapo Man United.”

Paul Scholes aliandika kwenye Instagram akimwambia Amorim kwamba kiungo Mainoo anastahili kuanza, aliposema: “Dogo anaharibiwa, kushindwa kucheza kwenye timu ambayo inashindwa kutawala mchezo wa soka. Nachukia kuona wachezaji waliozalishwa kwenye klabu wanaondoka, bila shaka ni wakati wake sasa kuondoka, inatosha.”

MECHI ZIJAZO ZA MAN UNITED

-Desemba 15 vs Bournemouth (nyumbani)

-Desemba 21 vs Aston Villa (ugenini)

-Desemba 26 vs Newcastle (nyumbani)

-Desemba 30 vs Wolves (nyumbani)

-Januari 4 vs Leeds United (ugenini)

-Januari 7 vs Burnley (ugenini)