Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rosenior apewa mtego Chelsea

Muktasari:

  • Mabosi wa The Blues walimjadili kocha huyo (41) baada ya kutolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na PSG kwa jumla ya mabao 8-2 baada ya mechi ya mkondo kufungwa mabao 5-2 kabla ya Jumanne kupigwa mabao 3-0.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Chelsea, Liam Rosenior ni kama anategwa na mabosi wa timu hiyo ambao licha ya kumjadili na kuamua aendelee na timu hadi mwisho wa msimu, lakini inaelezwa akifuzu tu huenda akasakwa kocha mpya.

Mabosi wa The Blues walimjadili kocha huyo (41) baada ya kutolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na PSG kwa jumla ya mabao 8-2 baada ya mechi ya mkondo kufungwa mabao 5-2 kabla ya Jumanne kupigwa mabao 3-0.

Hata hivyo, inaelezwa huenda Rosenior akaendelea kuwepo katika kikosi hicho kwa muda mrefu licha ya kujadiliwa na mabosi wa timu hiyo na kuamuliwa aendelee kuwepo hadi mwisho wa msimu.

Baada ya kichapo hicho cha aibu nyumbani, kulikuwa na wasiwasi kuhusu kocha huyo huenda akatimuliwa, lakini matokeo ya kikao cha mabosi hao kiliamua amalizie msimu kabla ya kujadiliwa tena.

Hata hivyo, kocha huyo aliyerithi mikoba ya Enzo Maresca aliyetimuliwa wiki 10 zilizopita, huenda akaendelea kuwepo zaidi endapo Chelsea haitafuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na mabosi wanataka kumpa muda wa kutosha ajenge kikosi imara na huenda akatimuliwa kama itafuzu ili kupata kocha atakayeiongoza vyema katika michuano hiyo mikubwa Ulaya.

Baada ya kuanza vizuri katika kikosi hicho, hivi karibuni Rosenior  amekuwa akipitia panda shuka nyingi kuanzia ligi ya ndani na michuano ya kimataifa na inaelezwa kwa sasa hakuna mpango wowote wa kumfukuza kabla ya msimu kumalizika, licha ya baadhi ya mashabiki  kutaka aondoke.

Vigogo wa Chelsea wanaona kumfukuza kwa sasa hakutakuwa na maana, hasa kutokana na ukosefu wa makocha wanaoweza kuchukua mikoba yake, huku pia msimu ukikaribia kumalizika.

Chelsea inapambana kurudi Ligi ya Mabingwa msimu ujao na katika msimamowa Ligi Kuu England iko nafasi ya sita na pointi moja nyuma ya Liverpool yenye 49 ikiwa nafasi ya tano, huku ikiamini chini ya kocha huyo itafuzu na kwa sasa haitaki kumpa presha ikiisaka tiketi hiyo muhimu.

Inaelezwa pia kushindwa kufuzu Uefa kutasababisha pia kuondolewa kwa baadhi ya nyota wake muhimu akiwamo Enzo Fernandez anayetakiwa na Real Madrid.