Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rooney ataka Salah apigwe benchi

Muktasari:

  • Salah ambaye ameipa Liverpool mataji ya Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa misimu tofauti, huku akionyesha kiwango bora, kwa sasa anaonekana mzigo na hana maajabu tena katika kikosi hicho.

LIVERPOOL, ENGLAND: LEJENDI wa Manchester United, Wayne Rooney amesema winga wa Liverpool, Mohamed Salah inatakiwa akae benchi kwa sababu kwa sasa hana msaada katika timu hiyo.

Salah ambaye ameipa Liverpool mataji ya Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa misimu tofauti, huku akionyesha kiwango bora, kwa sasa anaonekana mzigo na hana maajabu tena katika kikosi hicho.

Salah, 33, aliyefunga mabao 29 na kutoa asisti 18 msimu uliopita wakati kikosi cha Arne Slot kilipochukua ubingwa wa EPL na msimu huu ana mabao manne tu katika ligi hiyo.

Kwa mwenendo wake wa sasa, umekuwa mjadala hasa kwa wachambuzi wa soka na nnyota wa zamani wa England, Rooney amependekeza Kocha wa majogoo hao, Arne Slot kufanya uamuzi mgumu wa kumweka nje nyota huyo wa kimataifa wa Misri.

"Kama ningekuwa Slot, ningefanya uamuzi mgumu ili kuisaidia timu. Kwa sasa Salah hana msaada hasa kwenye kulinda na kushambulia. Mfano ukiwa mchezaji mpya uko benchi na unamwona akikataa kukimbia na ni mchezaji wa hadhi kubwa na aliyefanya makubwa kwa klabu, ni ujumbe gani anakupa? Siyo picha nzuri. Slot ana kazi kubwa ya kuwarudisha wachezaji kwenye hali ya ushindi. Kubwa zaidi ni wanapopata matokeo mabaya kama haya, jina la Jurgen Klopp kila mara linatajwa, ni kama ilivyokuwa kwa Sir Alex Ferguson, wakati David Moyes na Louis Van Gaal walipokuja, jina la Fergie lilikuwa likitajwa mara zote timu inapofanya vibaya," alisema Rooney.

Wakati huo huo, mchezaji wa zamani wa Liverpool, Jamie Carragher alisema umefikia wakati Salah anatakiwa kuzungumza.

"Virgil Van Dijk baada ya mechi amekuwa akitoka na kuongea kama inavyotakiwa kwa nahodha, lakini wachezaji wengine pia wanapaswa kujitokeza kuongea kwa niaba ya klabu. Mwaka mmoja uliopita, Mo Salah hakuwa na hofu kuongea kuhusu masilahi yake binafsi, alisema kuhusu klabu kutompa mkataba," alisema Carragher na kuongeza;

"Mara nyingi kumsikia Salah akiongea ni pale anaposhinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mechi au anapohitaji mkataba mpya. Ningependa kumwona akitoka kama mmoja wa viongozi, mmoja wa magwiji wa Liverpool na kuongea kwa niaba ya timu. Haipaswi kuwa kazi ya nahodha kila mara."