Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ronaldo kufanya kikao na mabosi wa Al Nassr

RONALDO Pict

Muktasari:

  • Ronaldo aligoma kucheza mechi hiyo kwa kile kinachotajwa kuwa amechoshwa na tabia za mabosi wanaomiliki Al Nassr ambao anaona hawatoi pesa za kutosha kuhakikisha timu hiyo inafanya usajili.

RIYADH, SAUDI ARABIA: HIVI karibuni kumekuwa na sintofahamu katika kikosi cha Al Nassr baada ya Cristiano Ronaldo kugoma kucheza mechi dhidi ya Al-Riyadh mapema wiki hii.

Ronaldo aligoma kucheza mechi hiyo kwa kile kinachotajwa kuwa amechoshwa na tabia za mabosi wanaomiliki Al Nassr ambao anaona hawatoi pesa za kutosha kuhakikisha timu hiyo inafanya usajili.

Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno mwenye umri wa miaka 40 aliamua kugoma ili kuonyesha kuchukizwa kwake na mfuko wa Uwekezaji wa Umma wa Saudi Arabia (PIF) ambao unamiliki timu hiyo, Al Hilal na Al Ittihad.

Al-Hilal ilipewa ruhusa kumsajili beki wa zamani wa Arsenal, Pablo Mari, kutoka Fiorentina, pamoja na Kader Meite na Saimon Bouabre kwa pamoja katika madili yaliyogharimu Pauni 26 milioni kwa kila mchezaji.

RONA 01

Wakati huo huo, Al Nassr ilipewa fungu la kusajili mchezaji mmoja tu Januari, ambaye ni Haydeer Abdulkareem, 21, licha ya kocha Jorge Jesus kuomba kuongezewa wachezaji katika maeneo mengi.

Vilevile wapinzani wao, Hilal walipewa fungu la kumsajili Karim Benzema, jambo lililozidi kumkera sana Ronaldo na kuamini kwamba Al Nassr hailindwi vya kutosha na PIF.

RONA 02

Kugoma kwa Ronaldo kuliibua tetesi kwamba kuna asilimia nyingi za kuondoka na ikizingatiwa katika mkataba wake ambao umebakisha misimu miwili, kuna kipengele kinachomruhusu kufanya hivyo ikiwa timu inayomhitaji italipa Pauni 43 milioni.

Hata hivyo, Sky Sports imeripoti kwamba, mabosi wa Al Nassr pamoja na PIF waliwasiliana na Ronaldo baada ya kugoma na walifanya naye kikao kumhakikishia kuwa kila kitu kitakuwa sawa katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Baada ya kikao hicho, kilichodumu kwa zaidi ya saa mbili, Ronaldo aliwaelewa na kukubali kusitisha mgomo wake na atacheza mechi dhidi ya Al-Ittihad.

Muda mchache baada ya kikao, Ronaldo, alichapisha picha yake akiwa amevaa jezi ya mazoezi ya Al-Nassr, akiambatanisha na emoji za mioyo ya njano na bluu rangi za jezi ya nyumbani ya Al-Nassr.

RONA 03

Hadi sasa, Al Nassr, yenye maskani yake jijini Riyadh ipo nyuma kwa pointi moja tu dhidi ya vinara wa Ligi Kuu, Al-Hilal.

Ronaldo amefunga mabao 18 katika mechi 22, akikosa kufunga katika mechi nne tu za ligi.

Licha ya jambo hilo kuonekana kutulia kwa sasa, Ronaldo anatazama kwa makini kuona nini kitatokea katika dirisha lijao la majira ya kiangazi ikiwa timu hiyo itasajili wachezaji wakali au laa na ikiwa itakuwa tofauti kuna uwezekano mkubwa akaomba kuondoka baada ya michuano ya Kombe la Dunia.