Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rekodi hii ya Mbappe Madrid, Ronaldo akasome

Muktasari:

  • Straika huyo amefunga mabao 13 kati ya mabao 21, ambayo Madrid imefunga katika hatua ya makundi ya michuano hiyo, jambo ambalo halikuwahi kufanywa na mchezaji yeyote Real Madrid, hata mfungaji bora wa muda wote wa UEFACL, Cristiano Ronaldo.

Zaidi ya nusu ya mabao ya Real Madrid katika Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu yamefungwa na Kylian Mbappe, huu ni wastani mkubwa zaidi wa mabao kufungwa na mchezaji mmoja katika historia ya klabu hiyo.

Straika huyo amefunga mabao 13 kati ya mabao 21, ambayo Madrid imefunga katika hatua ya makundi ya michuano hiyo, jambo ambalo halikuwahi kufanywa na mchezaji yeyote Real Madrid, hata mfungaji bora wa muda wote wa UEFACL, Cristiano Ronaldo.

Mbappe ambaye usiku wa Jumatano amefunga mabao mawili wakati timu yake ya Madrid ikishushwa kwa nafasi 6 hadi ya tisa katika msimamo wa Ligi ya Mabingwa baada ya kipigo cha mabao 4-2 kutoka kwa Benfica, amecheza mechi 7 kati ya nane ambazo timu yake imecheza katika hatua ya makundi akitumia dakika 621,  hana asisti, hana kadi ya njano wala nyekundu.

Madrid kwa kutolewa katika Top 8, ambazo zinaingia hatua ya 16-Bora moja kwa moja, sasa italazimika kucheza mechi mbili za play-offs ili kutinga hatua hiyo ya mtoano.

Timu nane za juu zilizofuzu moja kwa moja hatua ya 16-Bora na pointi zake katika mabano ni Arsenal (24), Bayern (21), Liverpool (18), Tottenham (17), Barcelona (16), Chelsea (16), Sporting (16), Manchester City (16). Madrid imemaliza nje ya Top 8 ikiwa na pointi 15 katika nafasi ya 9.