Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ronaldo ajibu ishu ya Joao Felix

Muktasari:

  • Katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi, Felix, mwenye umri wa miaka 25, aliachana na Chelsea na kujiunga na Al Nassr ya Saudi Arabia, wakati ambao timu kibao barani Ulaya zilitamani kumsajili.

RIYADH, SAUDI ARABIA: STAA wa Ureno, Cristiano Ronaldo amekosoa maoni ya watangazaji wa kipindi kimoja cha Youtube waliokosa uhamisho wa Joao Felix kwenda Al Nassr.

Katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi, Felix, mwenye umri wa miaka 25, aliachana na Chelsea na kujiunga na Al Nassr ya Saudi Arabia, wakati ambao timu kibao barani Ulaya zilitamani kumsajili.

Felix aliungana na nyota mwenzake kutoka Ureno, Ronaldo, ambaye yupo kwenye klabu hiyo tangu mwaka 2023.

Katika msimu wa 2024/25, Felix alicheza mechi 20 chini ya Kocha  Enzo Maresca na kufunga mabao saba kisha alipelekwa kwa mkopo AC Milan Januari mwaka huu kabla ya kuuzwa kwenda Al Nassr kwa dau la Euro 30 milioni.

Hivi karibuni, kipindi cha mdahalo kiitwacho Chuveirinho kilikosoa  uamuzi wa Felix kuachana na soka la Ulaya na kuhamia Mashariki ya Kati, licha ya umri wake kuwa mdogo.

Katika sehemu ya maoni, Ronaldo alijibu kwa kuandika: "Hawa hawaelewi chochote kuhusu mpira, lakini bado wanatoa maoni yao."

Katika mahojiano yake na GOAL, Felix alipoulizwa kuhusu ushawishi wa Ronaldo kwenye uamuzi wake wa kujiunga na Al Nassr, alisema: "Ronaldo? Unaona wazi anajitahidi sana kuhakikisha soka la hapa linakua. Alikuwa mmoja wa watu wa kwanza kuzungumza nami kuhusu kuja hapa na alipozungumza nami nilihisi muda mzuri na nilivutiwa na hilo lilinisaidia kunishawishi."

Aliendelea: "Ninahisi ligi hii inakua sana. Kila mwaka, wachezaji zaidi wanakuja kucheza hapa. Mkakati wa Al Nassr ni mzuri na wa kusisimua. Nataka kusaidia klabu hii kadiri niwezavyo, kufunga mabao, kutoa pasi za mabao, na kuwasaidia kushinda mechi. Na muhimu zaidi, nataka kusaidia timu kushinda mataji. Hii pia ni kawaida yangu timu yoyote ninayocheza, huwa najaribu kufanya bora zaidi. Najaribu kuwasaidia wachezaji wenzangu na kusaidia klabu ninayoitumikia."

usiku wa jana Jumamosi, Al Nassr iliumana na Al Riyadh katika mechi ya Ligi Kuu Saudi Arabia kwenye Uwanja wa Al Awwal Park.