Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rodrygo, Leao wamzuzua Arteta, awataka Arsenal

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Mikel Arteta amekuwa akijenga kikosi  kwa muda sasa na ameripotiwa kufanya hadi mazungumzo binafsi na Rodrygo ambaye anaonekana kutokuwa na furaha katika kikosi cha kwanza cha Madrid kutokana na kukosa nafasi kubwa ya kucheza katika kikosi cha kwanza.

ARSENAL imeonyesha kuvutiwa kwa muda mrefu na winga wa Real Madrid na timu ya taifa ya Brazi,  Rodrygo mwenye umri wa miaka, 24, pamoja na winga wa AC Milan na Ureno Rafael Leao, 26, na inataka kuwasajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Mikel Arteta amekuwa akijenga kikosi  kwa muda sasa na ameripotiwa kufanya hadi mazungumzo binafsi na Rodrygo ambaye anaonekana kutokuwa na furaha katika kikosi cha kwanza cha Madrid kutokana na kukosa nafasi kubwa ya kucheza katika kikosi cha kwanza.

Arsenal kwa sasa inamtegemea sana Bukayo Saka na Gabriel Martinelli kwenye eneo la pembeni, hivyo inataka kuwasajili Leao na Rodrygo ili kuongeza ushindani wa namba na kuliboresha eneo hilo kwani Saka na Martinelli wakikosekana huwa pengo lao linaonekana.

Rodrygo ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028, ameonekana kupata nafasi kubwa ya kucheza katika mechi za hivi karibuni tofauti na ilivyokuwa wakati msimu unaanza.

Hata hivyo, uwezekano wa staa huyo kuondoka bado unaonekana kuwa mkubwa kwani licha ya kuanza kuchezeshwa inadaiwa bado ameendelea kuwa katika kundi la wachezaji ambao bado hawapendezwi na mbinu za kocha Xabi Alonso.

Kwa upande wa Leo, Milan inaonekana kuwa tayari kumuuza lakini inahitaji zaidi ya Euro 60 milioni ili kufanya hivyo, kiasi ambacho hakionekani  kuwa kikubwa sana kwa Arsenal.


MARC GUEHI

MKURUGENZI wa michezo wa Bayern Munich, Max Eberl, anapanga kufanya mazungumzo na wawakilishi wa beki wa kati wa Crystal Palace na timu ya taifa ya England Marc Guehi  ili kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya baridi mwakani.

Mchezaji huyu mwenye umri wa miaka 25 anaweza kusaini mkataba wa awali na klabu ya nje ya England ifikapo Januari kwa sababu mkataba wake utakuwa umebakisha miezi sita kabla ya kumalizika mwisho wa msimu huu.


YVES BISSOUMA

TOTTENHAM inapanga kumuuza kiungo wao wa kimataifa wa Mali Yves Bissouma katika dirisha lijalo la usajili la Januari.

Hata hivyo, mkataba wa fundi huyu mwenye umri wa miaka 29  unatarajiwa kumalizika katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Ikiwa itashindwa kumuuza katika dirisha lijalo, Spurs imepanga kutumia kipengele kilichopo katikq mkataba wake ili akae kwa mwaka mmoja zaidi.

Bissouma alijiunga na Spurs akitokea Brighton mwaka 2022 na amekuwa na vipindi vya mpito, akishindwa kuonyesha kiwango kilichotarajiwa mara kadhaa.


HARVEY ELLIOTT

ASTON Villa imeiambia Liverpool kwamba inapanga kumrejesha kiungo wao timu hiyo Harvey Elliott ambaye anacheza kwa mkopo katika kikosi chao.

Mabosi wa Villa wanataka kuachana na fundi huyu kwa sababu hajaonyesha kiwango walichotarajia tangu ajiunge nao katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22  alionekana kuwa ni hazina kwa Liverpool lakini kiwango chake kimezidi kushuka siku hadi siku.


SERGIO RAMOS

MANCHESTER United imekanusha tetesi zinazodai kwamba wapo katika mazungumzo na beki wa zamani wa Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania, Sergio Ramos ambaye kwa sasa anaichezea Monterrey ya Mexico mapema mwezi huu.

Ramos mwenye umri wa miaka 38,mkataba wake na Montrrey unatarajiwa kumalizika mwisho wa mwezi ujao na ripoti zinadai hana timu hiyo haina mpango wa kuurefusha zaidi, hivyo itaachana naye.


PHILIP OTELE

BOURNEMOUTH inamtazama winga wa  FC Basel, Philip Otele mwenye umri wa miaka 26, kama mmoja kati ya wachezaji wanaoweza kuziba pengo la staa wao Antoine Semenyo anayetarajiwa kuondoka katika dirisha lijalo la majira ya baridi ambapo vigogo wengi wameonyesha nia ya kutaka kumsajili.

Semenyo ambaye anahusishwa sana na Liverpool inayomwangalia kama mbadala wa Salah ni miongoni mwa mastaa wanaofanya vizuri katika Ligi Kuu England tangu msimu uliopita.


JOAO GOMES

KIUNGO wa Wolves, Joao Gomes yupo tayari kujiubga na  Manchester United  katika dirisha lijalo la majira ya baridi ambapo ripoti zinadai anaweza akanunuliwa kwa Pauni 44 milioni.

Staa huyu wa kimataifa wa Brazil  mwenye umri wa miaka 24, amevutiwa sana na mipango ya kocha Ruben Amorim ambaye amekuwa akizungumza naye kwa muda sasa akimshawishi ajiunge na timu hiyo.

Mkataba wa sasa wa staa huyu anatarajiwa kumalizika mwaka 2028.


YUSUF AKCICEK

TIMU mbalimbali barani Ulaya zinadaiwa kuihitaji saini ya beki wa kati wa Fenerbahce na timu ya taifa ya Uturuki, Yusuf Akcicek mwenye umri wa miaka 19, kuelekea dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Miongoni mwa timu zinazohitaji huduma yake ni pamoja na Tottenham Hotspur, Bayern Munich, Atletico Madrid, Napoli na RB Leipzig.

Maskauti wa timu hizi wanadaiwa kuonekana mara kwa mara katika mechi za Fenerbanhce kwa ajili ya kutazama maendelea ya beki huyo.