Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rodrygo afichua kilichombakisha Real Madrid

RODRYGO Pict

Muktasari:

  • Rodrygo, alihusishwa kuondoka Real Madrid, huku klabu kama Manchester City, PSG, na Arsenal zikiripotiwa kuonyesha nia ya kumchukua. Hata hivyo, amebaki Santiago Bernabeu na sasa anapigania kurejesha nafasi yake ya kuanza kwenye kikosi cha Xabi Alonso.

Nyota wa Real Madrid, Rodrygo, amefichua mazungumzo aliyofanya na kocha Xabi Alonso kufuatia hatima yake klabuni hapo wakati wa majira ya kiangazi na kuamua kubaki. 

Rodrygo, alihusishwa kuondoka Real Madrid, huku klabu kama Manchester City, PSG, na Arsenal zikiripotiwa kuonyesha nia ya kumchukua. Hata hivyo, amebaki Santiago Bernabeu na sasa anapigania kurejesha nafasi yake ya kuanza kwenye kikosi cha Xabi Alonso.

Mchezaji huyo kutoka Brazil amesema haikuwa rahisi kubaki Real Madrid, kwani kulikuwa na mazungumzo ya mara kadhaa na kocha huyo ambaye walikubaliana baadhi ya mambo ili kuendelea kuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo.

Amesema alikubali mpango wa kocha huyo wa kumtumia katika nafasi tofauti, japokuwa yeye hupendelea kucheza kama winga wa kushoto.

RODR 01

Akizungumza na gazeti la AS, Rodrygo amekiri kuwa anapenda kucheza upande wa kushoto, lakini lengo lake kubwa ni kupata muda zaidi wa kucheza na anafahamu kuwa hawezi kupata dakika nyingi katika nafasi hiyo anayoipenda. 

Ameongeza kuwa yuko tayari kuisaidia Real Madrid katika nafasi yoyote, ambayo kocha atahitaji acheze.

"Xabi alipofika, aliniita na kuniambia, najua unapenda kucheza kushoto, lakini nitakuhitaji katika nafasi nyingine pia.

"Nikamjibu, sawa kocha, nipo hapa kuisaidia timu. Kila mtu anajua napendelea kucheza upande wa kushoto na nafanya vizuri zaidi upande huo, lakini niko tayari kucheza kulia au kama namba tisa, nilimwambia hivyo."

Ameongeza: "Kweli ni kwamba amenichezesha upande wa kushoto tu, na napenda muda ninaopata uwanjani. Nafanya vizuri, japokuwa kwa kawaida ningependa kucheza zaidi. Niko kwa lolote ambalo kocha wangu ataamua, ninazidi kuwa bora kila wakati, na ninajisikia furaha. Ninaonesha kiwango bora zaidi kila mara."

Katika hatua nyingine, Rodrygo amesema kwamba jukumu la mchezaji uwanjani ni kutoa uwezo wake wote kila anapopewa nafasi, iwe ameanza mechi au ameingia akitokea benchi. 

RODR 02

Amesisitiza kuwa anataka kutumia kila nafasi anayopata kikamilifu akiwa na jezi ya Real Madrid.

"Kama umeanza mechi, lazima utoe asilimia 100 lakini hata ukiingia kama mchezaji wa akiba, ni hivyo hivyo. Ndivyo ninavyofikiri. Kama nitacheza dakika 20, nitatoa kila kitu katika muda huo. Hilo linaboresha taswira yangu na linasaidia timu pia. Ninajaribu kutumia kila dakika ninayopata nikiwa na jezi ya Real Madrid," Amesema.

Rodrygo amecheza jumla ya dakika 129 pekee kwenye mechi sita za La Liga msimu huu. Katika Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League), amecheza mechi mbili, akitoa asisti mbili, lakini kwa jumla amecheza dakika 83 tu kwenye mashindano hayo.